Na Kassim Nyaki, NCAA.
Nchi ya Tanzania kupitia Jiopaki pekee iliyoko kusini mwa jangwa la Sahara ya Ngorongoro-Lengai, ambayo inatambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imekabidhiwa u-Rais wa mtandao huo katika kikao cha 10 cha Kidunia cha UNESCO Jiopaki kinachofanyika katika mji wa Marrakesh, Nchini Morocco.
Ujumbe kutoka Tanzania ulioko Nchini Morocco kupokea heshima hiyo umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu), Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Dkt. Freddy Manongi.
Rais Mpya wa Mtandao wa Jiopaki Afrika aliyechaguliwa ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mhandisi Joshua Moshi Mwankunda ambaye ni Meneja wa Idara ya Urithi wa Utamaduni na Jiolojia NCAA.
Faida kubwa ambazo nchi ya Tanzania itazipata kupitia uongozi wa mtandao huo ni pamoja na;
1. kuongezeka kwa muonekano chanya wa nchi ya Tanzania kimataifa,
2. Kuongezeka kwa idadi ya watalii na watafiti watakaotembelea nchi ya Tanzania kwa Shughuli mbalimbali.
3. Kupanua wigo wa mashirikiano ya kimataifa katika sekta ya uhifadhi na utalii wa jiopaki na miamba (Geopark)
4. fursa ya kuongeza vivutio vingi vya utalii wa miamba kupitia uanzishwaji wa jioapaki mpya nchini Tanzania.



Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mhandisi Joshua Mwankunda (kushoto) akikabidhiwa cheti cha kuwa Rais wa Mtandao wa Jiopaki Barani Afrika kutoka kwa Rais anaemaliza muda wake Bw.Driss Achbal kutoka Nchini Morocco katika vikao vinavyoendelea Nchini Morocco kuanzia tarehe 9 Septemba, 2023
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...