Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WASHINDI kedekede wameendelea kujinyakulia fedha taslimu sanjari na Simu janja (Smartphones) kupitia promosheni ya Maokoto Deilee ya Sportpesa na Tigo ambayo tayari imeingia kwenye wiki ya pili.

Tandale jijini Dar es Salaam, droo ya pili ya promosheni hiyo ilifanyika hadharani na mshindi wa shilingi Milioni moja (Tsh. 1,000,000/-) alitangazwa kutoka mkoa wa Iringa sanjari na mshindi wa simu janja (smartphone) wa mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Sportpesa, Sabrina Msuya amesema wataendelea na droo hiyo kwa kushirikiana na Tigo hadi atakapo tangazwa mshindi wa mwisho ambaye atashinda kiasi cha shilingi Milioni Kumi na Tano (Tsh. 15,000,000).

“Tunasisitiza kwa wateja wetu kuendelea kubashiri na Sportpesa kupitia mtandao wa Tigo (Tigopesa), wakiweka fedha zao kupitia mtandao wa Tigo wanao uwezo wa kubashiri michezo mbalimbali kupitia Sportpesa,” amesema Msuya.

Mwakilishi wa Mtandao wa Tigo, Afisa Biashara, Fabian Felician amewahimiza wateja mbalimbali kuendelea kubashiri michezo mbalimbali kupitia tigopesa huku akisisiza kuwa wataendelea kutoa zawadi za fedha na simu janja kushirikiana na Sportpesa.

Promosheni hiyo ya Maokoto Deilee kila siku inatoa kiasi cha shilingi Elfu Ishirini (Tsh. 20,000/-) kwa wateja wanaobashiri na Sportpesa kupitia Tigopesa, kila wiki inatoka Simu janja (smartphone) na shilingi Milioni moja (Tsh. 1,000,000/-) na kubwa kuliko ni Tsh. 15,000,000/-.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...