Na Habib Miradji

TANZANIA imeshauriwa wakuza mitaala wake kufanya jitihada kubwa ya kuongeza somo la matumizi ya akili bandia katika kila hatua ya elimu ili kulinusuru taifa na matumizi mabaya yasiyoendana na mila, utamaduni na maadili ya taifa.

Ushauri huo umetolewa na Profesa Bekir Karlin wa Chuo Kikuu cha McGill  nchini Albania kwenye kongamano lililoendeshwa na Asasi ya Kilimanjaro Dialogue Institute ya jijini Dar es Salaam wakati akichangia mada juu ya Mchango wa Akili Bandia katika kudumisha maadili na amani duniani.

 Profesa Bakir alisema matumizi ya akili bandia hayakwepeki na mataifa yanapaswa kuwekeza kwa vijana wadogo kwani ni sawa na kuwakunja samaki wakiwa wabichi na hivyo kitawarahisishia   kujenga maadili na kuufanya ulimwengu wa amani na utulivu.

Profesa huyo alisisitiza Tanzania ina nafasi kubwa hasa katika kipindi hiki kunakofanyika mageuzi makubwa ya ukuzaji mitaala yake ili kuhakikisha somo la matumizi ya akili bandia linapewa nafasi yake kwa taasisi zote za elimui za umma na za binafsi.  Kwa kufanya kizazi kijacho kitapata maendeleo makubwa.

Awali, Rais wa Asasi ya Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI), Ibrahim Yunus Rashid, katika akifungua kongamano hilo, alisema matumizi ya Teknolojia kwa njia ya kompyuta na simu yameongeza, hivyo hapana budi mataifa kubuni mbinu za kuwalinda vijana  kuwa salama na  muhimu pia  wakilinda na tamaduni zao.

Yunus ambaye mtaalam wa masuala ya elimu, alieleza kutokana na uzoefu wake,  mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye sekta aliyoiongoza kwa zaidi ya miaka 20, yanatokana na jinsi ya kuhusisha akili bandia na masuala mbalimbali yahusuyo maisha na  nyezo hiyo imetumika kujenga vijana waadilifu.

Akichangia mdahalo huo uliofanyika kwenye ukumbi wa American Corner, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa, Bi Catherinerose Barretto wa Binary Institute of Technology (BIT) juu ya umuhimu wa kushirikisha jinsia bila ubaguzi unavyoweza kuchangia malezi na mwenendo chanya miongoni mwa vijana.

Alionya wazazi wengi hudhani matumizi ya akili bandia hudumaza watoto katika kufikiri lakini hali ya sasa ya matumizi ya mitandao ya kijamii  watoto na wazazi wana fursa sawa licha ya mitaala kutozalisha stadi stahiki na kuwepo kwa tofauti ubaguzi wa kidigitali kwa jinsia, rangi na hata kimiundombinu.   

Barretto alisema dunia haipaswi kuwa na woga. Suala ni kujenga maisha ya baadaye ni kukabili changamoto na kuwa tayari kutengeneza milima tunayoweza kuipanda.  

 Kalebu Gwalugano ambaye ni  Mkurugenzi Mkuu wa Neurotech alilitetea kundi la vijana ambalo ndilo msingi wa mageuzi katika matumizi ya akili bandia. Alitahatharisha kwa kundi hili ndilo linalokabiliwa na utandawazi wa kubeba tamaduni zisizokubalika.

 Amewataka vijana kutumia akili bandia kwa kuleta amani na sio mfarakano duniani, huku akisema viongozi wa kitaifa wakiweka mazingira muafaka wa kisheria. 

Bi Catherinerose Barretto wa Binary Institute of Technology akiwasilisha mada ya juu ya mchango wa akili bandia katika ujenzi wa maadali na amani Duniani
Mwenyekiti wa Kilimanjaro Dialogue Institute KDI Ibrahim Yunnus akiwasilidha Madame juu ya matumizi ya akili bandia katika ujenzi maadili na amani duniani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...