Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (kushoto), akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Hassan Babu (katikati), alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambapo anafanya ziara ya siku mbili mkoani humo kusikiliza changamoto mbalimbali wanazopitia wafanyabiashara na kuhamasisha matumizi sahihi ya mashine za Kieletroniki (EFD). Kulia ni Mbunge wa Moshi Mjini, Bw. Priscus Tarimo.
Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Tixon Tuyangine Nzunda (kulia), na Kamishna Msaidizi wa Uchambuzi wa Sera wa Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja (katikati), wakiwa katika kikao cha Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (hayupo pichani) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Hassan Babu (hayupo pichani), katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mjini Moshi.Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro, katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambapo anafanya ziara ya siku mbili mkoani humo kusikiliza changamoto mbalimbali wanazopitia wafanyabiashara na kuhamasisha matumizi sahihi ya mashine za Kieletroniki (EFD).Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (kushoto), akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Hassan Babu (kulia), baada ya mazungumzo yao, yaliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mjini Moshi, ambapo pia anafanya ziara ya siku mbili mkoani humo kusikiliza changamoto mbalimbali wanazopitia wafanyabiashara na kuhamasisha matumizi sahihi ya mashine za Kieletroniki (EFD).
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Kilimanjaro)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...