Morogoro

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Manispaa ya Morogoro inaendelea na matengenezo ya barabara ili wananchi waweze kusafiri kwa urahisi.

Hayo yameelezwa na Meneja wa TARURA Wilaya ya Morogoro Mhandisi Mohamed Muanda alipokuwa akielezea utekelezaji wa miradi ya Wakala katika Manispaa  hiyo.

Mhandisi Muanda amesema mkakati uliopo ni kuhakikisha kwamba barabara zote za lami zilizojengwa muda mrefu zaidi ya miaka ishirini na kupelekea kuchakaa pamoja na kuwa na mashimo ya mara kwa mara (port holes) zinafanyiwa matengenezo makubwa na madogo.

“Kama mnavyofahamu Manispaa ya Morogoro ni njiapanda na barabara zake  zinapitisha magari makubwa na madogo  pande zote za nchi , sisi kama TARURA tumeona njia hii ni nzuri na itasaidia kuziongezea muda wa kuendelea kuishi ili kutoa huduma kwa muda mrefu”

Mhandisi Muanda ameongeza kuwa aina hiyo  ya matengenezo ya barabara kwa kuongeza tabaka jingine la lami ( Overlay) kwa kuanzia wanaziba kwanza viraka vinavyotokea katika kila barabara na baadae wanachagua barabara moja ambayo inakua imezidiwa kutokana na kupitisha magari mengi na hivyo kuiongezea tabaka lingine la lami kwa juu.

Kwa upande wa kufungua barabara Mhandisi Muanda amesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa bajeti ya barabara imeongezwa kutoka Bil. 2.8 hadi kufikia Bil. 7.35 na kuwawezesha kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili wananchi.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...