Katika jitihada za kufungua biashara hususan ya nyama inayotoka Tanzania kwenda nchini Misri, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega  amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo kutoka nchini Misri, Mhe. El Sayed El Kosayer ili kuona uwezekano na kuweka mazingira wezeshi ya biashara hiyo baina ya nchi hizo mbili.

Waziri Ulega alifanya mazungumzo hayo na Mhe. El Kosayer  kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Pamoja na kujadiliana mambo mengine, suala la biashara ya nyama kutoka Tanzania kwenda kuuzwa nchini Misri lilijadiliwa kwa kina huku  Mhe. El Kosayer akiahidi kulifanyia kazi kwa haraka  ili biashara hiyo iweze kuleta matunda kwa pande zote mbili.

Mapema wakati wa mazungumzo yao, Mhe. Kosayer alimueleza Waziri Ulega kuwa lengo la kukutana kwao ni kuona namna wanavyoweza kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi ili ziweze kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...