Kwa mara ya kwanza nchini, wanafunzi wa kike wasiosikia (viziwi) 22 wa shule za sekondari ambao ni sehemu ya wanafunzi wa kike zaidi ya 150 wa shule za sekondari mkoani Arusha wamepatiwa mafunzo ya kutengeneza tovuti na ‘coding’.

Ikijulikana kama ‘Code Like a Girl’, jitihada hizi zinachangia kutengeneza mustakabali endelevu zaidi jumuishi na wa kidigitali barani Afrika huku ikianisha changamoto ya uwakilishi mdogo wa wanawake katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM) kupitia mpangilio wa programu maalaum ya kielimu inayowalenga wasichana wasio na uwezo.

Ikiwa ni programu ilianzishwa na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC, Meneja Maendeleo ya Rasilimali Watu wa kampuni hiyo ya mawasiliano na teknolojia, Bw. Naiman Moshi amewaambia waandishi wa Habari mwishoni mwa wiki ambapo mafunzo hayo yamefanyika kuwa programu inalenga kutengeneza na kuleta shauku kuhusu masomo yanayohusiana na sayansi (STEM) kwa wasichana.

Amebainisha kuwa kupitia mpango huu, ambao ulianzishwa mwaka 2018, wanafunzi wa kike wanapatiwa fursa ya kufahamu hatua za awali na msingi za ‘coding’ na njia za kufuata kwa taaluma zinazohusiana na ujuzi wa sasa na ujao huku wakitengeneza vipaji ambavyo vinaainisha mahitaji ya maarifa yanayohitajika sasa na baadae.

“Kama kampuni ya teknolojia na mawasiliano, tumeamua kufanya jitihada hizi kwa lengo la kupunguza pengo lililopo kwenye maarifa ya kidigitali miongoni mwa wanafunzi wa kike,” alielezea Bw. Moshi, wakati akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kumalizika kwa mafunzo yaliyofanyika kwa siku nne katika Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC).

Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) linakadiria kwamba ni 35% pekee ya wanafunzi wote wanaojiunga na masomo yanayohusiana na Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM) ni wanawake.

Kupunguza pengo la kijinsia lililopo katika sayansi pia ni muhimu kwa mafanikio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Shirika la Umoja wa Mataifa na kufanikisha ajenda ya kufikia mwaka 2030 ya “kutomwacha mtu yoyote nyuma”.

Programu hii, ambayo pia inatekelezwa kwa kushirikiana na Tanzania Data Lab (dlab), imefanikisha kuona zaidi ya wanafunzi wa kike 1900 ambapo wengine ni walemavu wakijiunga na mafunzo haya, kwa dhamira ya kufanikisha dhana ya ujumuishi.

Mratibu wa Programu kutoka dlab, Bi. Somoe Mkwachu, ameelezea kuwa bado kuna jitihada za kimakusudi zinahitajika kufanyika katika kuainisha dhana potofu ya kwamba “masomo ya sayansi ni kwa ajili ya wavulana” na kusaidia kupunguza pengo la kijinsia lililopo katika masomo ya sayansi.

“Jitihada hizi ni sawa na tone la maji kwenye bahari, inahitajika kuongeza kiwango cha maarifa ya kidigitali ambapo kwa sasa ni suala linalogusa kila Nyanja,” aliongezea.

Mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya sekondari ya Ngarenaro, Dorcas Prima ameelezea kufurahishwa kwake kushiriki katika mafunzo haya, akisema kwamba yatasaidia kuongeza uelewa wake, hususani katika masomo yanayohusiana na sayansi.

Kupitia programu hii, wanafunzi wanajifunza maarifa yanayohusu ‘coding’ na kupata fursa ya kukutana na marafiki wapya pamoja na washauri wa kitaaluma.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...