Baadhi ya wakimbiaji wa baiskeli wa Km.60 wakiwa katika picha  ya pamoja na Mwenyekiti  wa Taasisi  ya Utu Kwanza Wakili Msomi Shehzada Walli mara baada  ya kuwasili katika  viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Kutoka Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Pauline Gekul  akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi  ya Utu Kwanza  Wakili Msomi Shehzada Wali  mara baada ya kuwasili viwanja vya Leaders  baada ya kumaliza mbio za Km 60 kutoka Bagamoyo hadi Dar es Salaam leo asubuhi Septemba 10, 2023 anayepiga makofi ni Mkurugenzi wa Kampuni ya MOIL Atlaf Hiran Mansoor.
Mwenyekiti  wa Taasisi  ya Utu Kwanza akiwa katika picha ya pomoja na baadhi ya wafanyakazi wake ambao ndiyo wameandaa Utu Kwanza Fun Run.



Matukio mbalimbali.

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MWENYEKITI wa Taasisi ya Utu Kwanza Wakili Msomi Shehzada Wali amesema kuwa wamejipanga kuanzisha mradi ambao unaitwa Nyumbani Salama wenye lengo la kuwatetea watoto ili waweze kupata haki ya kuwaona wazazi wao ambao wanatumikia vifungo mbalimbali Gerezani.

Wakili Msomi Shehzada amesema hayo leo Septemba 10,2023 katika kilele cha Utu Kwanza Fun Run ambapo yeye binafsi amekimbia umbali wa Kilometa 60 kutoka Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani hadi Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, Dar es Salaam, pia kulikua na mbio za baiskeli na wengine wamekimbia Km5, Km10 na Km21.

Wakili Msomi Shehzada amesema kuwa wapo wafungwa Gerezani wa kike ambao huwa wajawazito na wanapojifungua husababisha ongezeko la watoto wa mitaani kutokana na watoto hao kukosa muda wa kuishi na mama zao hivyo watazungumza na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili ikiwezekana kuwekwe utaratibu maalumu ambapo watoto waweze kwenda Gerezani kuwaona wazazi wao tofauti na ilivyo sasa.

Mbali na hilo pia Utu Kwanza tayari wameshazindua mradi wa dawati ambalo litakwenda kuzungumza na wafungwa waliopo Gerezani wa rika zote ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za kisheria sambamba na kutambua haki zao za msingi licha ya kuwa watuhumiwa ama wafungwa.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Usambazaji mafuta ya Moil Fuelling Atlaf Hirani Mansoor ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Utu Kwanza Run amesema kuwa anatoa pongezi kwa Tasisi ya Utu kwanza kwa kuweza kulikumbuka kundi ambalo lilisahaulika katika miaka ya nyuma, kila mwananchi anayo haki ya kufahamu haki zake hata kama anakuwa ni mkosaji kwani wapo wengine wako Gerezani kwa kesi za kusingiziwa ila kwakua hawana familia zenye uwezo na wengi hawatambui haki zao tunaimani kubwa hili dawati la Utu Kwanza litakwenda kutatua hii changamoto.

"Naupongeza uongozi wa awamu ya sita wa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi pamoja na sekta binafsi kwani wote tunajenga nchi moja" amesema Atlaf Hiran Mansoor.

"Serikali ya awamu ya sita ni sikivu pia wakati tunakimbia binafsi nimeongea na Naibu Waziri, Sheria na Katiba Pauline Gekul amesema kuwa hili wazo la Utu Kwanza walikua nalo miaka mitatu nyuma ila kwakuwa wao wamelianzisha basi hawana budi kuwapa ushirikiano wa kutosha." Amesema Mkurugeni wa MOIL Mansoor.

Ameahidi kushirikiana na Taasisi ya Utu Kwanza katika juhudi hizi nchi nzima ambako watakwenda kuanzisha dawati la msaada huu kwa jamii".

Kassim Lila aliyeibuka mshindi wa kwanza wa Km.60 amesema kuwa anashukuru Mungu amemaliza mbio hizo salama bila kuumia pia amewashukuru Utu Kwanza kwa kumpa sapoti kubwa pia ameongeza kwa kusema kuwa dawati hili la msaada limekuja katika wakati miafaka kwani waliojaa magerezani ni vijana ambao wengi wao hawana msaada hivyo ana matumaini makubwa kwamba watasaidika.

Mgeni rasmi katika Utu Kwanza Fun Run Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul amesema kuwa Tume ya Jaji Mstaafu Othman Chande ambayo imefanya kazi kubwa kwa kuzunguka nchi nzima, Bara na Visiwani imekusanya nawazo kwa wananchi na wadau wote wa Sheria ili kuboresha Mfumo mzima wa Haki Jinai nchini.

Ndiyo maana Wizara ya Sheria na Katiba hatukusita kupokea wito na kushiriki kwenye hafla hii ya Utu Kwanza baada ya kuridhishwa na malengo na kazi nzuri inayofanywa na Shirika hili la Utu Kwanza sambamba na jitihada za Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha maisha ya watanzania wote bila kujali rangi, itikadi, jinsia wala asili kwenye sekta ya upatikanaji wa haki na hasa Haki Jinai ambako ndiko linapopatikana Kundi la Mahabusu na Wafungwa.

Utu Kwanza jina hili limebeba maana kubwa na pana sana kwa kifupi linamaanisha Ubinadamu Kwanza hivyo ni matarajio ya Wizara na Serikali kwa ujumla kuona kuwa Shirika hili linaendeleza malengo yake kwa mujibu wa Sheria za nchi katika kulinda na kuboresha utu na thamani ya binadamu katika upatikanaji wa Haki Jinai.

Sisi kama Wizara tunasema wadau mbali mbali wa Sheria na Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayojihusisha msaada wa Sheria nchini kutumia rasilimali zake vizuri ili kuwafikia walengwa na kushirikiana na serikali katika kuboresha maisha ya watu wote.

Utu uendelee kuwa kipaumbele chetu kwenye Haki Jinai na sote tutatimiza wajibu wetu katika kuwatumikia Watanzania na kudumisha amani na nshikamano ambazo ni tunu muhimu kwa maendeleo na ustawi wa taifa letu.

Wizara ya Sheria na Katiba inatambua na kuthamini mchango mkubwa na jitihada za Shirika la Utu Kwanza katika kuboresha maisha na Utu wa wafungwa na mahabusu katika kipindi cha miaka sita tangu kuanzishwa kwake kwa kuwafikia mahabusu na wafungwa katika baadhi ya Magereza hapa nchini, hasa Jijini Dar es Salaam.

"Hongereni sana kwa kuanzisha mradi wa Dawati la Msaada wa Sheria ( Legal Aid Desk) mnapata sababu nyingine ya kusherehekea mafanikio makubwa ya kazi yenu katika kuweka maslahi ya Utu Kwanza kwa vitendo. Tukio hili la Utu Kwanza Run halisaidii tu afya na kuwaleta wanajamii pamoja bali pia nimeambiwa linasaidia kuchangisha fedha kwa ajili ya mradi huu na kwa niaba ya Mhe. Waziri Dkt. Pindi Chana tutawachangia kiasi cha Mil.2

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...