Na Mary Margwe,  Geita

WADAU mbalimbali wanaoomba fedha kwaajili ya Mazingira wametakiwa kuhakikisha fedha wanazoomba wanazitumia  kwenye eneo lililokusudiwa na si kufanya ujanja ujanja unaopelekea kukwamisha harakati za Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ambayo inahamasisha utuzaji wa Mazingira,kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Ruthberta Supply  Ruthberta Myonga amesema hayo  leo Septemba 22 Mwaka huu Mkoani Geita kwenye Maonyesho ya 6 ya  Teknolojia Madini yanayofanyika katika Viwanja vya  Bombambili.

Myonga amesema wapo wadau wanaojitokeza kuomba fedha kwa ajili ya utunzaji wa Mazingira lakini chakushangaza fedha hizo haziendi kwenye lengo lililokusudiwa, Hali inayopelekea kukwamisha juhudi za Serikali ya amamu ya sita.

" Wadau wa Mazingira tuhakikishe fedha tunazoomba zinakwenda kutumika  kwenye eneo husika ili kurudisha Imani ya wanaotufadhili, na sio kufanya  ujanja ujanja unaopelekea kukwamisha harakati za Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ambayo inahamasisha utuzaji wa Mazingira, kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini " amesema Myonga

 Aidha Myonga ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wanawake kote nchini kupanda miti mbalimbali ya matunda  na kivuli Kwa lengo la kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi

Amesema kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi Kuna umuhimu wa kuhakikisha kila Mtanzania anashiriki kikamilifu upandaji miti ikiwa pamoja na kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na wadau wa Mazingira.

" Mbali na kupanda miti ya matunda pia wajikite katika kupanda miti ya maua na hiyo ni kutokana na Fursa inayopatikana katika miti ya maua ambapo itawasaidia kujikwamua kiuchumi" amesema Myonga.

Amesema Ruthberta Supply ipo katika Maonyesho hayo lengo kubwa likuja ni kuwahamasisha Watanzania juu ya umuhimu wa kupanda miti na kutunza Mazingira huku ikimbukwe kuwa  kuna changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo ni muhimu kwa kila Mtanzania kupanda na kutunza Mazingira kwenye maeneo yanayozunguka.

" Ruthberta Kampuni tupo katika Maonyesho haya lengo kubwa nikuja kuwahamasisha Watanzania juu ya umuhimu wa kupanda miti na kutunza na ikimbukwe kuwa hivi Sasa Kuna changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo ni muhimu Kwa kila Mtanzania kupanda na kutunza Mazingira kwenye maeneo yanayozunguka "amesema Myonga

" Hivi sasa  katika Mikoa ya Kanda ya ziwa ikiwemo Mkoa huu wa Geita kumekuwa na muamko mkubwa wa watu kupanda miti ya matunda na hata hapa mmeona watu mbalimbali wanavyokuja Kwa wingi kuuliza na kununua miti kwani wamejua umuhimu wa kupanda miti na kwamba tunahamasisha zaidi kupanda miti ya matunda, miti dawa, na miti ya kivuli." Amesisitiza  Myonga.

Myonga pia ametoa shukrani kwa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mazingira kwa kuwaunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau ikiwa pamoja na kutoa matamko mbalimbali yanayohamisisha upandaji wa miti na kupitia Kampuni yake watahakikisha wanaongeza kasi ya kuelimisha Watanzania pamoja na kuzalisha miti kwa wingi ili kila Mwananchi apande miti hiyo, na hatimaye kuweza kunufaika na matunda, kivuli.

Myonga ameongeza kuwa  Kampuni licha ya kuwataka Watanzania kupanda miti lakini pia wanahakikisha wanafuatilia masuala ya Mazingira ili kupata taarifa zake kwa lengo la kuona miaka 200 ijayo itakuwa imepungaza  kasi ya ukataji miti.

Kufuatia hilo  Myonga anawaalika wakazi na wananchi wa Mkoa wa Geita kutembelea katika Banda lake ili kuona aina mbalimbali za miti ukiwemo ukwaju wenye radha kama ya tende ambao pia unatiba ndani yake na mapera mekundu ambayo kilo Moja ambayo mbegu yake ni endelevu.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...