Na Elias Gamaya, Shinyanga, Septemba13, 2023,

MAHAKAMA kuu ya Tanzania Divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi masijala ya Shinyanga hii imendelea kusikiliza kesi ya ugaidi na uhujumu uchumui kwa shahidi wa 5 kesi namba 3 ya mwaka 2023 inayosikilizwa na jaji Geofrey Isaya.

Akitoa ushahidi wake shahidi wa 6 aliyepewa jina la P kutokana na kesi yenyewe amesema mnamo januari 2017 alipewa taariifa na kiongozi wake juu ya uwepo wa vikundi hiyo vya kigaidi katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake ambapo alipewa jukumu la kuja kufanyia kazi taarifa hiyo ya kiiterijensia ambapo aliondoka Jijini Dar es salaam na kufika mkoani Shinyanga ndipo alipobaini uwepo wa kundi la kigaidi wilayani kahama mkoani Shinyanga .

Kutokana na taarifa za kiinterijensia alifika wilayani kahama baada ya kufanya uchunguzi wake ndipo alipobaini kuwepo kwa kundi hilo la kigaidi linaloswali msikiti wa Swadikin uliopo maeneo ya Shunu wilayani Kahama ambapo aliamua kujiunga kuswali na waumini wa msikiti huo kwa muda wa mwaka mmoja na mwezi mmoja ili kufanya uchunguzii wa kina zaidi kuhusiana na taarifa hizo za kiiterijensia.

Shahidi huyo amesema kwa muda ambao aliswali kwenye msikiti huo wa Swadkin Mawaidha na hotuba ambazo zilikuwa yanatolewa na amir wa msikiti huo ambaye ni salim Haluma mshitakiwa wa Kwanza katika kesi hii yalikuwa yanalenga kufanya hijira na Jihadi pamoja na kujiandaa kujiunga na makundi ya kigaidi ikiwemo Al shabaab, Isilamic state pamoja na boko haram ili kujiandaa kupindua nchi ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Shahidi huyo ameenda mbali na kusema kwa kipindi alichoswali pamoja na waumini hao kunamichango ambayo ilikiwa inachangishwa na viongozi wao itakayowasaidia kununua Silaha za kivita kwa ajili ya kujiandaa na vita ya kupindua serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambapo kutokana na michango hiyo amiri Salim Haruna aliteua watu wawili kwenda kununua silaha hizo nchini Burundi
silaha aina ya Bunduki mbili SMG na mabomu mawili.

Kesi hii shauri namba 3 ya mwaka 2023 itaendelea kusikilizwa kesho septemba 14, 2023 kwa shahidi wa 7upande wa Jamhuri kesi inayowakabili washitakiwa nane kwa makosa sita 1,Kupanga njama ya kuvyamia vituo vya polisi kwa kupora Silaha ambazo zingetumika kinyume cha sheria, 2 kuajili watu ili wajihusishe na vitendo vya kidaidi,   

3kukusanya fedha ambazo zingetumika kutendeka kwa vitendo vya kigaidi Tshs elfu 80,000/=, 4 kufadhili fedha kwa ajili ya kutendeka kwa vitendo vya kigaidi, 5 kukusanya fedha kiasi cha Tshs1,000,000/= kwa ajili ya kutumika katika vitendo vya kigaidi, 6 kushiriki vikao vinavyohusu kutendeka kwa vitendo vya kigaidi ilihali wakitambua vinakwenda kutishia Umma.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...