Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo wamezindua rasmi chapa mpya ya ligi ya daraja la kwanza (championship) ambayo kwasasa inafahamika kwa jina la NBC Championship hatua ambayo inatambulisha rasmi udhamini wa benki hiyo kwenye ligi hiyo.Tukio la uzinduzi wa chapa hiyo limekwenda sambamba na uzinduzi wa mashindano hayo ya soka yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Ujio wa chapa hiyo ni sehemu utekelezaji wa mkataba wa udhamini uliosainiwa hivi karibuni baina ya pande hizo mbili unaotoa fursa kwa benki hiyo kuendelea na udhamini wake kwenye ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara ‘NBC Premiere League’ hadi msimu wa 2027. Mkataba huo wenye thamani ya TZS 32.56 bilioni pia unajumuisha ligi za vijana kwa klabu zinazoshiriki ligi kuu ‘NBC Youth League’ na ligi ya daraja la kwanza "NBC Championship".

Tukio la uzinduzi wa chapa hiyo mpya limefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi waandamizi wa pande zote mbili na wadau wengine wa mchezo huo wakiwemo waandishi na wachambuzi wa habari za mpira wa miguu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC Elibariki Masuke alisema ni mwendelezo wa mkakati benki hiyo kuendelea kuiboresha ligi hiyo kwa kuendelea kuangazia misingi muhimu ikiwemo kukuza vipaji vya wachezaji na kuongeza ushindani kwenye mchezo huo uliofanikiwa kuteka hisia za wananchi wengi hapa nchini.

"Ni wazi kwamba kwasasa mchezo wa soka hususani ligi yetu imegeuka kuwa sit u kivutio cha burudani kwa mamilioni ya wapenda mchezo huu bali pia umekuwa ni jukwaa wezeshi la kijamii na kiuchumi, kwa kutoa fursa za ajira, kurahisisha shughuli za kiuchumi. Mafanikio haya yamekuwa muhimu sana kwetu sisi kama taasisi ya kifedha kwa kuwa yanatoa fursa kwetu kuhudumia kundi kubwa la wanamichezo na wadau wa sekta hii muhimu.’’ Alisema.

Kwa mujibu wa Bw Masuke ushirikiano huo baina ya benki hiyo na wadau wa mchezo wa soka nchini unathibitisha azma ya benki katika kuwakutanisha Watanzania na fursa mbalimbali huku akiahidi kwa niaba ya benki hiyo kuendeleza ukuaji endelevu wa soka na fursa za kiuchumi hapa nchini.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa (TFF), Boniface Wambura aliemuwakilisha Rais wa TFF Wallace Karia, pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa jitihada zake za kuendelea kuongeza udhamini wake kwenye mchezo huo alisema udhamini wa benki hiyo kwenye soka la vijana na daraja la kwanza ‘NBC Cjampionship’ utaimarisha pia ligi Kuu ‘NBC Premier League’ kutokana ongezeko la vipaji la ushindani unaotarajiwa kufutia uwekezaji uliofanywa na benki hiyo kwenye ligi hizo.

‘’Imekuwa ni bora zaidi kwetu kwasababu hii ni mara ya kwanza kupata mdhamini mmoja anaweka nguvu kwenye ligi zetu. Umuhimu wa hatua hii unaonekana zaidi katika urahisishaji wa maamuzi muhimu bila uwepo wa miingiliano ambayo muda mwingine ingeweza kutuchelewesha. Tunawashukuru sana NBC kwa kuona umuhimu wa kuchukua mnyororo mzima wa hizi ligi ambazo kiukweli zinategemeana sana…hivyo tunatarajia mafanikio zaidi kwenye soka letu,’’ alisema Wambura.

Kwa mujibu wa Wambura, mafanikio hayo ni ushahidi wa imani ya wadau mbalimbali nchini katika mchezo huo na viongozi wake kwa ujumla.


Mitano tena! Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC Elibariki Masuke (wa tano kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura (wa sita kutoka kulia) wakijipongeza sambamba na wafanyakazi wengine taaasisi hizo mbili mara baada ya kuzindua rasmi chapa mpya ya ligi ya daraja la kwanza (championship) ambayo kwasasa inafahamika kwa jina la NBC Championship chini ya udhamini wa benki hiyo. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Binafsi wa Benki ya NBC Elibariki Masuke akizungumza na wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa chapa mpya ya ligi ya daraja la kwanza (championship) ambayo kwasasa inafahamika kwa jina la NBC Championship chini ya udhamini wa benki hiyo. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa (TFF), Boniface Wambura akizungumza na wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa chapa mpya ya ligi ya daraja la kwanza (championship) ambayo kwasasa inafahamika kwa jina la NBC Championship chini ya udhamini wa benki hiyo. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mitano tena! Wafanyakazi wa Benki ya NBC akiwemo Mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo David Raymond (wa nne kulia) wakijipongeza mara baada ya kuzindua rasmi chapa mpya ya ligi ya daraja la kwanza (championship) ambayo kwasasa inafahamika kwa jina la NBC Championship chini ya udhamini wa benki hiyo. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...