Na Mwandishi Wetu , Dodoma

Serikali kupitia  Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma chini ya Wizara ya Fedha imewasilisha muswada wa mabadiliko ya sheria ya Ununuzi wa Umma yam waka 2023 ikieleza namna jinsi muswada huo unavyoweza kutatua changamoto zilizopo kwenye sheria iliyopo sasa ikiwemo suala la uekaji wa ukomo wa bei katika ununuzi wa baadhi ya bidhaa, huduma na kazi za ujenzi.

Akiwasilisha Muswada wa mabadiliko ya sheria hiyo Waziri wa fedha Mheshimiwa Dkt, Mwigulu Nchemba , Akiwa bungeni hivi karibuni Amesema kupitia Ibara ya 73 ya muswada huo umeelezea uwepo wa bei kikomo zitakazotumika  katika bidhaa, huduma na kazi za ujenzi ili kuepusha Ununuzi wa bidhaa au huduma fulani katika eneo moja kwa bei tofauti, jambo ambalo linapelekea ukosekanaji wa thamani halisi ya fedha kutokana na baadhi ya huduma au bidhaa kununuliwa kwa bei ya juu zaidi kuliko bei halisi ya soko.

“Mheshimiwa Spika, Muswada unapendekeza kuweka masharti kwa Taasisi nunuzi kununua bidhaa, huduma na kazi za ujenzi kwa kuzingatia bei kikomo ambazo zitaandaliwa kwa kuzingatia bei ya soko. Lengo ni kupunguza gharama kwa kutatua changamoto ya bei kubwa zinazotokana na ununuzi ambao hauzingatii bei halisi ya soko.” Amesema Dkt Nchemba

Aidha ibara hiyo pia imepambanua kuwa sheria haitasita kuchukuwa hatua za kinidhamu kwa mtumishi wa umma yeyote atakaefanya ununuzi wa bidhaa, huduma au kazi za ujenzi kwa bei ya juu kuliko bei kikomo zilizoelekezwa na Serikali kwa bidhaa au huduma husika.

“Hata hivyo, Mtumishi wa Umma atakayehusika na ununuzi wa bidhaa, huduma au kazi za ujenzi kwa bei ya juu kuliko bei kikomo, atachukuliwa hatua za kinidhamu. Aliongezea Dkr Nchemba.

Muswada huo wa mabadiliko ya sheria wa mwaka 2023 unalenga kuboresha sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011 ambao dhumuni lake kuu ni kuweka masharti bora ya usimamizi wa ununuzi wa umma, ugavi na uondoshaji wa mali kwa njia ya zabuni. Kwa ujumla, Sheria inayopendekezwa inakusudia kutatua changamoto zilizobainika katika utekelezaji wa masharti na taratibu za ununuzi, ugavi na uondoshaji wa mali kwa njia ya zabuni.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...