15.09.2023

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na Wananchi  wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 24 * kwa siku ya *Jumamosi Septemba 16, 2023 hadi  Jumapili Septemba 17, 2023.

Sababu: Kuruhusu matengenezo kwenye miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji ambayo yatasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji.

Maeneo yatakayoathirika ni; 

 Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Pichandege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti,Ubungo, Kisarawe, Ukonga, Pugu, Uwanja wa ndege, Majumba sita , Kiwalani na Gongo la Mboto na Kisarawe

Tafadhali kumbuka kuhifadhi maji ili kuweza kuyatumia kipindi cha matengenezo.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 

0800110064 (bure) au 

0735 202 121(WhatsApp tu)


Imetolewa na 

Kitengo cha Mawasiliano


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...