Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation imetoa elimu ya
matumizi sahihi na salama ya kupikia kwa baadhi ya koo za Kimasai
wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Utolewaji wa elimu ya matumizi
salama ya gesi katika Koo za Kimasai ni sehemu ya muendelezo ule ule wa
kampuni ya Oryx kubadilisha maisha ya watanzania kuachana na nishati
chafu na isiyo salama kwa matumizi ya kupikia na kuanza kutumia nishati
safi hasa gesi.
Wafanyakazi wa Oryx Gas wakiongozwa na Meneja wa
Masoko wa kampuni hiyo Peter Ndomba kwa kushirikiana na Doris Mollel
foundation wamefika katika nyumba za koo za Kimasai na kuwafundisha
matumizi salama ya nishati ya gesi.
"Tunafahamu jukumu ambalo
tunalo kama kampuni ni kuendelea kutoa elimu ya matumizi salama ya
majiko ya gesi, tumefanya hivyo katika makundi mbalimbali katika jamii
ya Watanzania na leo hii kwa kipekee mafunzo haya tunayoa kwa koo hizi
za Kimasai na tumetumia nafasi hii kuwapa elimu na kuwagawia bure
mitungi ya gesi na majiko yake."
Akieleza zaidi Ndomba amesema
wanamshukuru Mbunge wa Jimbo la Siha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya
Dk.Godwin Mollel kwa jitihada zake za kuwafikisha Oryx katika boma za
koo za Kimasai na kutoa elimu hiyo.
Amesisitiza Oryx itaendelea
na mkakati huo kwa koo nyingine zaidi ili jamii yote ya Watanzania
iweze kutumia nishati hiyo safi na bora kwa mapishi na kwamba utoa huo
elimu pia umeenda sambamba na ugawaji mitungi ya gesi 300 kwa kada ya
watumishi wa sekta ya afya wilayani Siha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...