Mwakilishi wa Sportpesa kutoka Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Lydia Solomon akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ZIMEBAKI wiki mbili pekee kupatikana mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 15 za Kitanzania kupitia Promosheni ya Maokoto Deilee ya Kampuni ya Sportpesa wanaoshirikiana na Kampuni ya Tigo.

Kama kawaida washindi kedekede wameendelea kumiminika kupitia promosheni hiyo ambapo kwenye droo ya nne iliyofanyika kwenye ofisi za Sportpesa, Dar es Salaam, wamepatikana washindi wengine watatu kutoka Kisarawe na Tanga ambao wameshinda simu janja (smartphone) na mshindi mmoja kutoka Dodoma ameshinda Tsh. Milioni moja

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwakilishi wa Sportpesa kutoka Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Lydia Solomon amesema zimebaki wiki mbili kwa promosheni hiyo kutamatika wakati kubwa kuliko Tsh. Milioni 15 zitapata mshindi.

Vile vile, Lydia amewaasa wateja wa Sportpesa kuendelea kubashiri michezo kupitia mtandao wa Tigo (Tigopesa), amesema wateja hao waendelee kufuatilia mitandao mbalimbali ya kijamii ya Sportpesa ili kujua zaidi kuhusu promosheni hiyo na droo zake mbalimbali.

Kwa upande wake, Meneja wa Biashara wa Tigopesa, Fabian Felician ameendelea kuwahimiza wateja wa Mtandao huo kuendelea kubashiri michezo mbalimbali kupitia tigopesa huku akisisiza kuwa wataendelea kutoa zawadi za fedha na simu janja kushirikiana na Sportpesa.

Promosheni hiyo ya Maokoto Deilee imebakisha siku 30 pekee, wakati kila siku inatoa kiasi cha shilingi Elfu Ishirini kwa wateja wanaobashiri na Sportpesa kupitia Tigopesa, kila wiki inatoka Simu janja (smartphone) na shilingi Milioni moja na kubwa kuliko ni ushindi wa Tsh. Milioni 15.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...