Na Said Mwishehe, Michuzi TV
JESHI la Polisi kupitia Chuo cha Polisi cha Taaluma Dar es Salaam wameingia masaini makubaliano ya ushirikiano kati yao na Uongozi Insitute lengo likiwa kutumia maktaba za Uongozi Istitute kupata vitabu vya kusoma ili kuongeza maarifa.
Akizungumza leo Septemba 27,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini makubaliano hayo Ofisa Mtendaji Mkuu Uongozi Insitute Dk.Kadari Singo amesema kupitia maelekezo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura umefika wakati jeshi hilo sasa kutumia mikakati ya kisasa katika kutekeleza majukumu yake.
“Njia mojawapo ya kufanya jeshi la polisi kuwa la kisasa ni kwa maofisa wake kuanza kutumia maktaba yetu kujifunza zaidi na kujua dunia inakwendaje.Tunafahamu Jeshi la Polisi linafanya shughuli mbalimbali za kimafunzo.
“Nyingine tunaita ukakamavu lakini nyingine ni kufikiri na kutumia akili nyingi na mojawapo ya akili unaipata katika vitabu.Taasisi ya Uongozi maktaba yetu tunayo machapisho zaidi ya 50,000 mengi yakiwa katika mtandao ambayo tunaita Digital.
“Pia Uongozi Insitute tuna maktaba mbili moja iko Dar es Salaam ikiwa na vitabu zaidi ya 11,000 na ile ya Dodoma inavitabu zaidi ya 6000.Lengo letu ni kuwezesha viongozi walioko serikalini na katika sekta binafsi na kiraia wapate fursa za kujiendeleza kwani vitabu hivi vinapoandikwa vinaandikwa na watu ambao wako mahiri wanauwezo mkubwa
“Kwa hiyo kiongozi anapopata fursa ya kusoma kitabu anapata maarifa mengi sana, sasa lengo letu ni kushirikishiana na taasisi mbalimbali ikiwemo Jeshi la Polisi ili kuhakikisha na wenyewe wanakuwa wanufaika wa maktaba zetu,”amesema Dk.Singo.
Ameongeza wanashirikiana na Chuo Kikuu cha Havard na Chuo cha Oxford ambao wanawapatia mararida na mapachapisho mengi ambayo yanataarifa nyingi huku akifafanua uamuzi anaofanya kiongozi unahitaji taarifa nyingi na nyingi ziko katika vitabu.“Ndio sababu tunawahamasisha na tunawasisitiza watumie maktaba zetu.”
Kuhusu muamko wa kusoma vitabu amesema unakwenda vizuri ila mitandao ya simu na mitandao ya kijamii imeleta changamoto duniani kwani watu wengi wamepunguza kupenda kusoma vitabu na simu zimekuwa kama ndio maisha yao.
Amesema kwa hiyo kuna kazi inatakiwa kufanyika ya kuwafanya sio viongozi peke yake lakini hata wanafunzi na watoto wapende vitabu.
“Miaka ya zamani mzazi alikuwa akisafiri anamletea mtoto zawadi ya kitabu lakini siku hizi mzazi anaona sifa kumletea simu badala ya kitabu.Kwa hiyo ni changamoto ya duniani.
“Sasa hivi duniani wanafikiria ni namna gani watamnyang’anya simu mfanyakazi, ndio mjadala unaoendelea, makongamano yameshaendeshwa na mjadala umekuwa wanafanyaje mfanyakazi aweke simu chini afanye kazi.
“Hatuwezi kunyang’anya lakini tunafanyaje aone simu sio kitu cha maana sana ili afanye kazi zake.Kwahiyo changamoto ya teknolojia inafaida zake na hasara zake.”
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam SACP Dk.Lazaro Mambosasa amesema wao kama Chuo cha Taaluma ya Polisi wanaendelea kuendesha kozi mbalimbali ambazo zimesajiliwa na zinatambulika.
“Tunaendelea na mafunzo kwa maofisa na wakaguzi wasaidizi ambao wanategemea kumaliza hivi karibuni kozi zao, hivyo hiki ambacho tumekifanya leo kuingia makubaliano itakuwa fursa sasa Polisi kutumia vitabu na machapisho mbalimbali yaliyopo Uogozi Istitute.
“kwa hiyo kwetu ni furaha kwani maktaba hii inakwenda kuondoa mkwamo wa watu kushindwa kujisomea kwa kukosa fedha za vitabu.Kupitia mtandao vitabu hivyo vitapatikana lakini tunayafanya haya wakati tumekamilisha kutengeneza mitaala ya diploma ya sheria.
“Tulikuwa na cheti cha sheria toka mwaka 1972 lakini sasa tunaanza kutoa mafunzo ya diploma ya sheria lakini hatuishi hapo tunakwenda pia kaunzisha digrii ya Sayansi ya Polisi ambayo haijakuwepo.
“Ni mara ya kwanza mitaala hiyo tumeitengeneza na imepitishwa na hiki tunachokifanya leo kinakwenda kujenga uwezo katika kusoma na kuwajengea uwezo watu wetu kupitia programu mbalimbali watakazisoma kupitia maktaba hii.”



.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya utiaji saini ya makubaliano ya ushirikiano kati ta Uongozi Institute na Jeshi la Polisi kupitia Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...