RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewaasa Watanzania waliokabidhiwa vyeti kwa Tajnisi kuendeleza utiifu wa sheria na kuendelea kusihi kwa kujiepusha na vitendo viovu ili wasipotoshe dhamira njema ya Serikali ya kupewa uraia wa Tanzania.

Dk. Mwinyi alitoa nasaha hizo Ikulu, Zanzibar alipowakabidhi vyeti kwa tajinisi Watanzania 3319, wahamiaji wasiohamishika baada ya kikidhi vigezo na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa raia halali nchini.

Rais Dk. Mwinyi aliwataka Watanzania hao kuipa heshima inayostahili hadhi waliyopewana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa raia, kwa kuwa raia wema.

“Kwa hakika ndugu zangu mna wajibu kwa pamoja tushirikiane kulinda na kudumisha amani tuliyonayo kwa faida yetu, tuliopo sasa na wale watakaokuja baadae” aliwaasa Watanzania hao

Rais Dk. Mwinyi aliwahakikishia Watanzania hao kuwa na haki zote baada ya kuthibitishwa uraia wao kama wanazostahili raia wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia, aliwaasa kuzitumia vyema haki na fursa hizo kwa kushiriki kikamilifu kwenye harakati za maendeleo kwa ustawi wa familia zao na Taifa kwa jumla na kuwataka ambao hawajajisajili kufanya hivyo kwa mamlaka husika.

“Natumia nafasi hii kutoa wito kwa ndugu zetu ambao kwa namna moja au nyengine hawajafika kwenye Ofisi za Uhamiaji kujiorodhesha, ni vyema wakaitumia fursa hiyo ili watambuliwe rasmi, Serikali zetu zimedhamiria kulimaliza tatizo hili kutokana na athari zake”. Aliwasihi Dk. Mwinyi

Sambamba na kuzitaka mamlaka za Serikali na Binafsi kuwapa ushirikiano Watanzania hao kwenye masuala mbalimbali kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na iongozo iliyopo kama wanavyofanyia Watanzania wengine.

Katika hatua nyengine Rais Dk. Mwinyi alitoa wito kwa Idara ya Uhamiaji, kuendelea kuziimarisha sheria zilizopo hususan Sheria ya uraia wa Tanzania kwa kuifanyia mapitio kwa madhumuni ya kuiwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowahusu wananchi na wageni wanaofika nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni Yussuf akizungumza kwenye hafla hiyo alizipongeza Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nay a Mapinduzi ya Zanzibar kwa busara zao za kuwasahe Watanzania hao kiasi cha milioni mbili kama kima cha kulipia uraia wao pamoja na kupongeza ushirikiano kwa Serikali mbili hizo kulifanikisha jambo hilo.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kukamilisha ahadi ya kuzitatua changamoto za Wanzania hao wahamiaji wasiohamishika tangu alipowaahidi mwaka 2020 kuitekeleza kwa vitendo ahadi yake ya kushughulikia changamoto za Watanzania hao.

Kwa upande wake, Kamisha Jeneral wa Uhamiaji Tanzania, Dk. Anna Makakala alisema jeshi hilo linajukumu la kuratibu masuala yote ya uhamiaji nchini yanayohusu raia wanaoomba uraia kisha kukabidhi kwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi.

Aidha alieleza Idara ya Uhamiaji Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilifanya zoezi la utambuzi kwa Watanzania hao mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Watanzania hao waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za kukosa haki zao za msingi kisheria zikiwemop hati za uraia, hati za kusafirikia na haki nyengine wanazopatiwa Watanzani halisi.

Jumla ya Watanzania 3319 wenye asili ya mataifa mbalimbali waliokua wahamiaji wasiohamishika wametambuliwa rasmi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa raia halali wa Tanzania. Miongoni mwao 3116 wanaasili ya Msumbiji, 147 wanaasili ya visiwa vya Komorao, watano kutoka Burundi na raia mmoja kutoka Jamhuri ya Rwanda, aidha watoto 1675 pia walitambukliwa

IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR
 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,akimkabidhi cheti Bi.Halima Idarous Adnan mwenye Asili ya Comoro,mkaazi wa Vikokotoni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi, leo katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 05/09/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,akimkabidhi cheti Ndg.Karan Mohamed Ali, mwenye Asili ya Comoro ,Mkaazi wa Kisimamajongoo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi, leo katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 05/09/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,akimkabidhi cheti Bw.Mohamed Mzee Mbaba mwenye Asili ya Comoro ,Mkaazi wa Mkunazini Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi, leo katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 05/09/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,akimkabidhi cheti Bi.Agness Benadicto Lucas,mwenye Asili ya Msumbiji mkaazi wa Kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pembe wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi,viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 05/09/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,akimkabidhi cheti Bw.Abalhassan Mohamed Farouk mwenye asili ya Comoro,Mkaazi wa Mkunazini Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi,viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 05/09/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa wananchi na waalikwa mbali mbali katika hafla ya kukabidhi vyeti vya Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi, katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 05/09/2023.
Maafisa wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania wakiwa katika hafla ya kukabidhi vyeti vya Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi, leo katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar,Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) .[Picha na Ikulu] 05/09/2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...