NA Andrew Chale  ZANZIBAR.

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,  Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amewatoa hofu wakazi wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja kufuatia shughuli za awali zinazofanywa za miradi ndani ya maeneo yao ikiwemo ujenzi wa barabara na tathimini maeneo ya uwekezaji ambapo amewataka wananchi kuwa na amani.

RC Ayoub ameyasema hayo katika ziara yake aliyoifanya katika Shehia tatu za Misufini, Mangapwani na Kidazini eneo la Bumbwini ambapo akijibu kero za wananchi waliotaka kujua hatima yao kabla na baada ya ujio wa miradi hiyo ambayo mengine ipo hatua ya awali.

"Tusianze kutuhumiana, na kusukumiana, bado taratibu zinaendelea kwenye hili tuwe na amani.

Suala la wananchi kukaa na wawekezaji kulipana fidia. Hili la uwekezaji ukiacha bandari, bado maeneo mengine hayajaainishwa hivyo tutulie." Amesema RC Ayoub.

Na kuongeza kuwa,  "Kupitia kamati tutakuja kwenu wananchi na kuwaelimisha- ili mapendekezo yenu yachukuliwe. Nikiwa kama Mkuu wa mkoa nitaendelea kusimama kuona haki zinalindwa, Rais wetu anapenda haki, na tutalisimamia wote." Amesema RC Ayoub.

Aidha, kuhusu ujenzi unaondelea: "Wageni wanaojenga barabara si wawekezaji bali ni wakandarasi na wamepewa mkataba na Serikali wajenge miundombinu ya awali kwamba wajenge barabara ya mzunguko wa urefu KM 24, kwa maana km12 kwenda na KM 12, kurudi.

Hata hivyo,  amejibu masuala mengine ikiwemo fidia ambapo amsema: Suala la fidia ya ardhi, fidia ya kifusi ipo katika mchakato na inafanyiwa kazi.

"Tathimini inaendelea kufanywa, zipo zilizokamilika na zipo ambazo Wizara ya fedha  tayari wamezifanyia kazi na zinapelekwa sehemu husika kwa fidia.

Hata baadhi ya wananchi wameomba maeneo yao ya makaburi kuona namna ya kuyabakisha maeneo yaliopo huku pia wakiiomba Serikali kutoa fursa kwa wakazi wa maeneo hayo kupewa fursa za kazi kwenye miradi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...