Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SHAHIDI wa 22 katika kesi ya Mauaji inayowakabili aliyekuwa mke wa Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake ameieleza mahakama kuwa, hakumfanyia mahojiano mtoto wa marehemu Allen, juu ya kifo cha mama yake  kwa sababu waliona ufahamu wake ulikuwa mdogo.

Amesema hata baada ya mama yake kuwa amefariki kwa kuchinjwa shingo na koromelo lake kukatwa kwa kitu chenye ncha kali, mtoto Allen hakujua kama mama yake amekufa alisema "mama amelala lakini amechafuka"

Shahidi huyo Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa polisi ((SSP) David Mhanaya ameeleza hayo leo Septemba 5,2023 mbele ya Jaji Edwin Kakolaki wakati akifafanua maswali (Re Examination) ya wakili wa serikali  Paul Kimweri baada ya kumaliza kujibu maswali ya dodoso (cross Examination) ya wakili wa utetezi Peter Kibatala

Washtakiwa katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka 2018 ni wifi wa marehemu, Aneth, mjane wa Bilionea Msuya; Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella.

Aneth alifariki dunia Kwa kuchinjwa shingoni ĺMei 25, 2016, usiku nyumbani kwake, Kibada Kigamboni, wilayani Temeke (wakati huo).

Shahidi Mhanaya alipoulizwa juu ya kutumia majina mawili dhidi ya mshtakiwa Revocutus Myella, alidai,  mshtakiwa kweli anaitwa Revocatus Muyella  a.k.a Ray lakini katika cheti chake cha kumaliza mafunzo ya Mgambo kiliandikikwa jina la Revocutus Mollel a.k.a Ray.

Ameendelea kudai  hakuona umuhimu wa kufanyia uchunguzi jina la Revocutus Mollel kwa kuwa nyaraka zake zilionyesha jina hilo na hata wakati anafanya upekuzi nyumbani kwa mshtakiwa alikuta kitabu cha bunduki Chenye jina la Revocutus Mollel ambapo baada ya upekuzi mshtakiwa alikubali kuwa majina hayo yote huwa anayatumia na hivyo hata yeye katika kuandika alijikuta anaandika Revocutus Mollel kwa sababu ya nakala hizo.

Akizungumzia maswali aliyoulizwa juu ya  ripoti ya taarifa ya polisi (first crime report) shahid Mhanaya amedai, hiyo ni taaria ya awali ya polisi ambazo ili ziwe tayari lazima ziwe zimefanyiwa uchunguzi wa kina.

Hata hivyo shahidi amedai, hata maelezo ya kwamba washtakiwa Getrude Mfuru,  Kombo Haji, Wilbroad Kkmaro, Twaha Almas na Amir Almas wakamatwe zilikuwa ni taarifa za awali lakini baada ya uchunguzi wa kina kufanyika ndipo washtakiwa sahihi wakakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Kesi hiyo inaendelea kesho Septemba 6,2023.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...