Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akikabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya Shilingi Milion 24.7 kwa Uongozi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya baada ya kukabidhi msaada wa tofali zenye thamani ya fedha hiyo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa jengo la upasuaji wa moyo na mishipa ya fahamu katika hospitali hiyo leo tarehe 11 Septemba, 2023.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akikagua eneo ambalo linajengwa jengo la upasuaji wa moyo na mishipa ya fahamu katika hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya mara baada ya kukabidhi msaada wa tofali zenye thamani ya Shilingi Milioni 24.7 kwa Uongozi wa hospitali hiyo leo tarehe 11 Septemba, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...