Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival ” ni kichocheo kikubwa katika kukuza ajira na utalii nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameyasema hayo wakati akihitimisha tamasha hilo lililoambatana na mbio za “Tulia Marathon” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

“Tamasha hili ni moja ya zao jipya la utalii wa utamaduni ambalo limekuwa ni chombo muhimu cha kukuza na kuhifadhi utamaduni wa Tanzania kupitia Ngoma za Asili” Mhe. Kairuki amesisitiza.

Amefafanua kuwa tamasha hilo limekuwa na manufaa makubwa kwa jamii na wasanii wa Ngoma za Asili kwa kusaidia kukuza na kutambulisha tamaduni za Tanzania, kutoa ajira pamoja na kuchochea ukuaji wa utalii katika jiji hilo kwa kuwavutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi.

Aidha, amesema Tamasha hilo ni mwendelezo wa jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na utekelezaji wa mikakati ya Serikali ya kuongeza mazao ya utalii.

Amewataka wadau na washiriki wa tamasha hilo kutumia fursa ya uwepo wa tamasha hilo kuwekeza katika shughuli mbalimbali za utalii kama vile wakala wa biashara za utalii, kujenga kambi za kulala wageni, kujenga hoteli, kumbi za mikutano na maeneo ya michezo mbalimbali mkoani Mbeya.

Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameiomba Serikali kuunga mkono tamasha hilo kwa lengo la kuhakikisha utalii unakua katika ukanda wa Nyanda za juu Kusini.

Tamasha la Ngoma za Asili lililoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust, lilianza tarehe 28 hadi 30 Septemba, 2023 lengo ikiwa ni kuenzi asili na utamaduni wa Mtanzania pamoja na kukuza zao jipya la Utalii wa Utamaduni hasa katika Nyanda za Juu Kusini.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akihitimisha Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia)akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa kikundi cha ngoma za asili cha ekigoma katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia)akiteta jambo na Mtoto mchezaji wa ngoma za asili kutoka kikundi cha ngoma za asili cha Utandawazi, Katondo Kebera (kushoto)katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimuonyesha vyakula vya kiutamaduni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wa pili kushoto) ,vilivyopikwa katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (katikati) akimkabidhi zawadi mshindi namba moja wa vyakula vya kiutamaduni katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya ORYX, Araman Benoit.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) wakicheza ngoma za asili katika katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

Meza kuu ikipiga makofi kuashiria kufurahia ngoma za asili zilizokuwa zikitoa burudani katika jukwaa kuu kwenye Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya. Wa tatu kutoka kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na viongozi wa Chama na Machifu.

Baadhi ya washiriki wa Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

Machifu kutoka Mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakifuatilia matukio katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akihitimisha Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kuhitimisha Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama “Tulia Traditional Dances Festival” lililofanyika leo Septemba 30,2023 jijini Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...