Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limefanikiwa kutoa elimu kwa umma ikiwa ni moja ya  ya Taasisi za Kiserikali zinazoshiriki maonesho yanayoendelea katika Kongamano la Wiki ya Pili ya Ufuatiliaji (U&T).

Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya AICC jijini Arusha yalianza tarehe 12 Septemba na kilele chake ni tarehe 15 Septemba, 2023. 

TASAC inashiriki maonesho hayo ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu kazi  na majukumu inayoyatekeleza kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415.

Wadau wote mnaalikwa kutembelea banda la TASAC katika eneo zilipo Taasisi zilizo chini ya Wizara Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi.span>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...