Na fauzia Mussa, Maelezo

 

WADAU wa maendeleo wamesisitiza kutolewa kwa elimu ya uandishi wa ripoti ili kuona ripoti zinazoandaliwa zinakwenda sambamba na utekelezaji wa miradi inayoendeshwa kwa kuonesha thamani halisi ya fedha zinazotumika.

 

Akifungua mafunzo kwa maofisa wa kamati za Wilaya za mradi wa viungo Ofisa mkuu wa mawasiliano wa mradi huo Saphia Ngalapi alisema ripoti nyingi zinazoandaliwa zinakuwa na mapungufu hasa ya kuonesha thamani ya fedha zilizotumika katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

 

Alisema Taasisi za Serikali na Binafsi zimekuwa zikitekeleza miradi mbalimbali inayotokana na matokeo ya ripoti ,hivyo ipo haja ya ripoti hizo kuzingatia mahitaji muhimu ili wafuatiliaji waweze kuzitumia kwa ufanisi na weledi.

 

“ ripoti hukusanya  taarifa muhimu ambazo hutumika katika shughuli mbalimbali ,hivyo bila ya kuwa na taarifa sahihi hatuwezi  kufikia malengo.”

  

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka washiriki hao kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo sambamba na kuwa mabalozi wazuri wa kwenda kuwafundisha wenzao ili kuona taaluma hiyo inaleta tija kwao na taifa kwa ujumla.

 

Akiwasilisha mada ya ukusanyaji wa takwimu na kuandika ripoti Ofisa ufuatiliaji na tathmini Malik Rashid alisema  datazinapokusanywa  husaidia kutumika katika kuandika ripoti kwa ukamilifu na kuwasaidia watumiaji kujua  maeneo muhimu ya kuanza kuyafanyia kazi.

 

Hivyo amewasisitiza maofisa hao kuzingatia mambo muhimu katika kuandaa ripoti ikiwemo  ubora na takwimu  zenye  taarifa sahihi,

 

Nae meneja utekelezaji mradi wa viungo Ali Saidi Juma alisema lengo la mradi huo  ni kuwaleta pamoja wadau wa kilimo cha mbogamboga   na matunda pamoja na kuongeza thamani  bidhaa hizo ili  kuongeza kipato cha wakulima wadogo wadogo.

 

Nao washiriki wa mafunzo hayo walishukuru kupatiwa mafunzo hayo kwani yatawasaidia kuongeza uwezo na uwelewa wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

 

Mradi wa viungo unatekelezwa kwa mashirikiano na taasisi tatu ikiwemo PDF,community, forest pemba (CFP) pamoja na Tamwa Zanzibar chini ya ufadhili wa umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Serikali ya Zanzibar kupitia Wizara ya kilimo.


Ofisa Mkuu wa Mawasiliano Mradi wa Viungo Safia Ngalapi akizungumza na maafisa  wa kamati za Wilaya za mradi wa viungo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo  maafisa hao juu ya  ukusanyaji wa takwimu na ustadi WA kuandika ripoti huko Ofisi za viungo Mwanakwerekwe Zanzibar.

Meneja utekelezaji wa mradi wa Viungo Ali  Said Juma  akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo  maafisa wa  kamati za Wilaya za mradi wa viungo juu ya  ukusanyaji wa takwimu na ustadi wa kuandika ripoti huko Ofisi za viungo Mwanakwerekwe Zanzibar

Ofisa tathmini na ufuatiliaji Maliki Rashid  akiwasilisha mada ya ukusanyaji wa Taarifa kwa maafisa  wa  kamati za Wilaya za mradi wa viungo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo  maafisa hao juu ya  ukusanyaji wa takwimu na ustadi WA kuandika ripoti huko Ofisi za viungo Mwanakwerekwe Zanzibar.

 

 PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...