Na Gift Thadey, Geita


GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba amewasihi wachimbaji wa madini nchini kutotembea na fedha taslim mifukoni badala yake watumie mifumo ya kielektroniki katika kutoa na kupokea fedha.

Gavana Tutuba ameyasema hayo Mjini Geita wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini.

"Nawashauri wachimbaji kutumia mifumo ya kielelektoniki kupokea na kutoa fedha badala ya kutembea na fedha taslimu," amesema Tutuba.

Gavana Tutuba amesema wao kama BOT wanalipa kwa mfumo wa TIPS ambao unarahisisha kwa kuwa umeunganishwa na mabenki yote na miamala ya simu nchini.

"Ndiyo sababu tunawahamasisha wachimbaji watumie mifumo ya kielektroniki kuliko fedha taslimu kwa kuwa ni mfumo wa haraka na una nafuu utawaepusha na fedha bandia," amesema Gavana Tutuba.

Amesema kuwa na mfumo wa kielektroniki ni nafuu zaidi hata kuepuka kuibiwa fedha tofauti na kuwa na fedha taslimu mkononi au mfukoni.
Gavana wa Benki Kuu (BOT) Emmanuel Tutuba akizungumza na waandishi wa habari Mjini Geita kwenye maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini. Picha na Gift Thadey

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...