Mkurugenzi Mtendaji wa Tech Hub Limited, Bw. Moses Lukoo akipanda mti aina ya mkoko kwenye eneo la Pwani ya Maweni, Mjimwema, Kigamboni jijini Dar es Salaam, ikiw ni kuhamasisha maadhimisho ya wiki ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu duniani.

Baadhi ya vijana wakishirikio zoezi la upandaji miti ya mikoko katika eneo la Serikali ya Mtaa Maweni ikiwa ni kuadhimisha wiki ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya milenia duniani.

Baadhi ya vijana wakishirikio zoezi la upandaji miti ya mikoko katika eneo la Serikali ya Mtaa Maweni ikiwa ni kuadhimisha wiki ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya milenia duniani.

Sehemu ya vijana walioshiriki zoezi la upandaji miti ya mikoko katika eneo la Serikali ya Mtaa Maweni wakiwa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya zoezi lao.


Baadhi ya vijana wakishirikio zoezi la upandaji miti ya mikoko katika eneo la Serikali ya Mtaa Maweni ikiwa ni kuadhimisha wiki ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya milenia duniani.

Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tech Hub Limited, Bw. Moses Lukoo, akiwa na timu yake na mshindi wa tuzo za UN SDG Action Awards, Bw. Emmanuel Mushy (wa pili kushoto)  wameungana na vijana pamoja wa wajumbe wa Serikali ya Mtaa Maweni katika kuadhimisha wiki ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya milenia duniani.

Baadhi ya vijana walioshiriki zoezi la upandaji miti ya mikoko pamoja wa wajumbe wa Serikali ya Mtaa Maweni katika kuadhimisha wiki ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya milenia duniani.

Washiriki wa  zoezi la upandaji miti ya mikoko pamoja wa wajumbe wa Serikali ya Mtaa Maweni katika kuadhimisha wiki ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya milenia duniani, wakiwa kwenye semina mara baada ya zoezi lao.

BAADHI ya Vijana wameshiriki zoezi la upandaji miti ya mikoko katika maeneo ya fukwe za Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kushiriki maadhimisho ya Wiki ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) duniani.

Zoezi hilo lililoratibiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tech Hub Limited, Bw. Moses Lukoo pamoja na mshindi wa tuzo za UN SDG Action, Bw. Emmanuel Mushy limeshirikisha vijana mbalimbali pamoja na wajumbe wa serikali ya Mtaa wa Maweni Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya tukio hilo la upandaji miti ya mikoko, Mkurugenzi Mtendaji wa Tech Hub Limited, Bw. Moses Lukoo alisem katika kuadhimisha wiki hiyo mambo mbalimbali yamefanyika ikiwemo kutoa semina juu ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, maarifa ya kijani kwa vijana.

Alisema vijana pia wamepatiwa elimu ya umuhimu wa utunzaji mazingira na kingo za bahari pamoja na elimu zaidi juu ya malengo ya maendeleo endelevu ya UN na mchango wa vijana katika utekelezaji wake. 

Kwa upande wake, Mshindi wa Tuzo za UN SDG Action, Bw. Emmanuel Mushy alisema pamoja na mambo mengine vijana waliojitokeza walifanya usafi wa kuokota plastiki eneo la bahari na kupanda miti ya mikoko eneo la Pwani ya Maweni, Mjimwema, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Alisema zoezi hilo ni endelevu na watakuwa wakihamasisha vijana kulifanya kila watakapokuwa na fursa na uwezo (uwezeshwaji) wa kufanyika. Jumla ya miti ya mikoko 50 ilipandwa katika fukwe hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...