Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI  wa Tasisi ya Fahari Tuamke maendeleo Neema Willgard Mchau ametoa msaada wa mahitaji muhimu wenye thamani ya Sh.milioni 2.7 kwa wanafunzi wenyechangamoto ya kusikia(Viziwi)katika Shule ya Msingi Mzambarauni mkoani Dar es salaam.

Msaada huo  uliotolewa kwa wanafunzi hao ni  sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika program ya ‘Tabasam na Mama’

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo Wilgard amesema wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa anaguswa na matatizo mbalimbali ya watoto wenye uhitajikwa kuwachangia gharama za matibabu na kuwapatia misaada.

“Fahari Tuamke maendeleo tumeamua kuendeleza program ya Tabasam na Mama kwa kuchangia mahitaji muhimu kwa wenye uhitaji na program hii kwetu itakuwa endelevu”amesema Wilgard.

Pia ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ofisi na Mkurugezi wa Almashauri pamoja  na Ofisi ya Ofisa Mtendaji wa kata  hiyo kwa kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kuwafikia watu wenye uhitaji.

Ametoa mwito kwa wakina mama kuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono Mhe Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya.

Awali Mkuu wa Shule ya Msingi Mzambarauni kingengo Maalum George Njau amemshukuru kwa msaada aliotoa kwa watoto hao na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano kwa kuwasaidia watoto wenye uhitaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...