Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewataka wafugaji wa asilia wilayani humo kuhakikisha wanafuga kisasa na kuacha kufuga kimazoea ili kuepuka athari zinazotokana na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi ambapo mifugo mingi hufa kwa kukosa malisho.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa soko jipya la mnada wa ng'ombe na mazao mbalimbali ya chakula lengo ni kukuza Uchumi wa wilaya hii na wafugaji hao kuuza mifugo kabla ya Kipindi cha ukame kuanza ni muda muafaka sasa wafugaji hao kutumia soko jipya la mnada Kirinjiko lililopo wilayani humo Kwa kuuzia mifugo yao.

DC Kasilda amesema Serikali imewawekea mazingira mazuri ikiwemo miundo mbinu ya kisasa kwa ajili ya kuendesha mnada katika eneo hilo.

"Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwakuelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya Maendeleo ikiwemo kwenye Sekta ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Afya, Elimu pamoja na miundombinu ya Barabara na Maji."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Anastasia Tutuba amesema mpaka sasa kwenye eneo hilo Halmashauri imeshapima vizimba zaidi ya 600 na halmashauri wataendelea kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana katika eneo hilo lengo likiwa ni kuiongezea Halmashauri mapato na kuinua uchumi wa wananchi wa Wilaya hiyo.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...