Septemba 19, 2023, ni siku ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anakwenda kuandika historia mpya katika sekta ya uvuvi kwa kuzindua ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko ambayo haijawahi kuwepo tangu nchi ya Tanzania ipate uhuru.

Hayo yamefahamika wakati, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa na ugawaji wa boti za kisasa za Uvuvi, Wilayani Kilwa, Mkoani Lindi leo Septemba 14, 2023.

Akiongea na waandishi hao wa habari, Waziri Ulega alisema hatua hiyo ya Rais, Dkt. Samia ya kuzindua ujenzi wa bandari hiyo ni ishara kwamba anakwenda kuandika historia mpya na kitendo hicho kinaonesha dhamira yake ya dhati ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi kupitia sekta ya uvuvi hapa nchini.

"Rais, Dkt. Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha sekta ya uvuvi inawafaidisha Watanzania wote hivyo uzinduzi huo atakaoufanya Septemba 19 mwaka huu inakwenda kusaidia kutoa majawabu mengi ya kiuchumi, ajira na kipato kwa Wananchi wa ukanda wa Pwani na Tanzania yote kwa ujumla," alisema Ulega

Alisema ujenzi huo wa bandari ukikamilika Watanzania takriban Milioni 5 watapata kipato chao kutokana na shughuli za uvuvi na zinazohusiana, ikiwemo pamoja utengenezaji wa boti, ukarabati wa nyavu, usindikaji wa samaki, na biashara mbalimbali ndogondogo.

Aliongeza kuwa ujenzi wa bandari hiyo unaashiria mwanzo wa enzi mpya za uvuvi wa kisasa Tanzania ambapo wakazi wa maeneo ya Pwani watapata ajira zaidi ya 30,000, fursa mpya za biashara na pia tekinolojia mpya.

Waziri Ulega aliendelea kufafanua kuwa uzinduzi wa bandari hiyo itakuwa ni mkombozi kwa sekta ya uvuvi kwani itawezesha Tanzania kuwa na nafasi kubwa katika soko la Kimataifa la Uvuvi, kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania na pia kuleta tija kwa wavuvi wadogo na wakubwa.

Kuhusu ugawaji wa boti za Uvuvi, Waziri Ulega alisema kufuatia mpango wa Wizara wa kutoa mkopo wa masharti nafuu wa Boti za kisasa za Uvuvi na vifaa vyake, unalenga kubadilisha maisha ya wavuvi, kutoa ajira nyingi zaidi, na kukuza uchumi wa Tanzania




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...