Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WASHINDI kedekede wameendelea kumiminika kupitia promosheni ya Maokoto Deilee ya Kampuni ya Sportpesa inayoshirikiana na Kampuni ya Tigo Tanzania, kupitia droo zao za kila wiki.

Droo iliyochezeshwa leo, kwenye ofisi za Sportpesa jijini Dar es Salaam, washindi wengine watatu wamepatikana ambapo wawili wamejishindia simu janja (smartphones) na mmoja ameshinda kiasi cha fedha taslimu shilingi Milioni moja.

Mwakilishi wa Sportpesa, kutoka Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Lydia Solomon amesema wamefanya droo hiyo huku akiwataja washindi wa simu janja, Felister Nyota kutoka Morogoro na Yohana Gilbert wa Manyoni, Singida huku mshindi wa Tsh. Milioni moja ni Boniface Boaz kutoka Dodoma.

“Promosheni yetu imebakiza siku 30 kuelekea mwisho wake kwa droo ya mwisho ambayo mshindi atashinda kiasi cha shilingi Milioni 15 (Tsh. 15,000,000/-) kwa kubashiri Sportpesa kupitia mtandao wa Tigo na tunaendelea kuwahimiza wateja kubashiri kujishindia kiasi cha shilingi elfu 20 kila siku, Simu janja na shilingi Milioni moja kila wiki,” amesema Lydia.

Kwa upande wake, Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Tigo, Fabian Felician ameendelea kuwahimiza wateja wa Mtandao huo kuendelea kubashiri michezo mbalimbali kupitia tigopesa huku akisisiza kuwa wataendelea kutoa zawadi za fedha na simu janja kushirikiana na Sportpesa.

Promosheni hiyo ya Maokoto Deilee imebakisha siku 30 pekee, wakati kila siku inatoa kiasi cha shilingi Elfu Ishirini (Tsh. 20,000/-) kwa wateja wanaobashiri na Sportpesa kupitia Tigopesa, kila wiki inatoka Simu janja (smartphone) na shilingi Milioni moja (Tsh. 1,000,000/-) na kubwa kuliko ni Tsh. 15,000,000/-.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...