Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka,  amezitaka  jamii za kiafrika na hasa wale wanao tumia lugha za asili kuendelea kuthamini lugha zao na hasa kupata maarifa ya namna lugha hizo zina thamani katika kulinda tamaduni mahalia.

Hayo ameyasema leo wakati akifungua warsha ya siku tano ya watafiti kutoka nchi 9 za Afrika na Ulaya (Uingereza, Ujerumani, Israel, Kenya, Ethiopia, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na mwenyeji Tanzania), yenye lengo la kujadili na kutafiti umuhimu wa lugha za asili kwenye masuala ya kuhifadhi kumbukumbu za tamaduni za watu. Warsha inafanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 04 hadi 08 Septemba, 2023, katika Ndaki ya Insia na Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu cha Dodoma.

Aidha, Prof. Kusiluka ameeleza umuhimu wa kufanya tafiti na kutunza historia ya makabila 120 ya Tanzania,  na kwamba tafiti zilizofanyika hadi sasa zimetupa changamoto ya kuheshimu lugha zetu, utamaduni wetu, na kwamba Chuo Kikuu cha Dodoma kitaendelea kufanya tafiti kwenye eneo hili, kwa lengo la kusaidia Serikali na Jamii kwa ujumla kutambua  umuhimu wa utunzaji wa maarifa ya lugha asili, na kuendelea kuenzi mila na tamaduni zetu tulizorithi kwa mababu.

 “Lengo la warsha hii ni kubalidilishana uzoefu kuhusu matumizi ya lugha katika kuhifadhi maarifa asilia na kuona kwa namna gani maarifa asilia yanaweza kutunzwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.” Alisisitiza  

Naye Mhadhiri wa lugha kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt. Chrispina Alphonce, ambaye pia ni mratibu wa warsha hiyo, amesema ni muhimu kwa jamii kujua kutumia maarifa  yaliyopo katika lugha zao za asili, kwani kuna faida nyingi katika kukuza utamaduni wa jamii husika na taifa kwa ujumla.

Washiriki wa Warsha hiyo pamoja kufanya mijada ya kina ya tafiti zilizofanyika pia watatembelea mkoa wa Manyara, ambako watakutana na makabila makubwa mawili Datooga na Wairaki na kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu namna gani wanalinda na kuenzi  lugha za asili, athari za mazingira na mwingiliano wa tamaduni unavyoathiri lugha za asili, elimu, utandawazi na matibabu ya magharibi yalivyochangia makabila hayo kupoteza asili.  

Matokeo ya warsha hiyo ni kuibuliwa kwa maeneo mengi zaidi ya utaifiti kusaidia nchi za Afrika kulinda tamaduni na lugha za asili sambasamba na utandawazi. Warsha hiyo imefadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Volkswagen la nchini Ujerumani, Chuo Kikuu cha Cologne Ujerumani  na Chuo Kikuu cha Dodoma.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, akifungua warsha ya kujadili na kutafiti umuhimu wa lugha asili kwenye uhifadhi wa kumbukumbu za tamaduni
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo- Taaluma, Utafiti na Huduma kwa Jamii akikakaribisha washiriki katika warsha ya kujadili na kutafiti umuhimu wa lugha asili katika uhifadhi kumbukumbu za tamaduni
Prof. Alice Michel mtafiti Mkuu wa utafiti wa lugha za asili katika uhifadhi wa kumbukumbu za tamaduni akielezea jambo kwa upana kwa washiriki.
Washiriki wa warsha ya kujadili na kutafiti umuhimu wa lugha asili kwenye uhifadhi wa kumbukumbu za tamaduni wakifuatilia warsha hiyo
Washiriki wa warsha ya kujadili na kutafiti lugha za asili katika uhifadhi wa kumbukumbu za tamaduni wakifuatilia warsha.

  

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka (wa nne kutoka kulia) katika picha ya pamoja na Washiriki wa warsha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...