Na Mwandishi Wetu, Tanga

WAZIRI wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu amekabidhi mitungi mikubwa ya gesi ya Oryx 150 pamoja na majiko yake bure kwa wanawake wajasiriamali 450 wa Jiji la Jiji la Tanga huku akitumia nafasi hiyo kuwataka wajiamini katika shughuli wanazofanya.

Akizungumza alipokuwa akikabidhi mitungi hiyo ya Oryx Gas Waziri Ummy ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Oryx na Cocacola kwa kutoa vifaa hivyo kwa wajasiriamali hao.

Ametumia nafasi hiyo kueleza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuthamini na kutambua mchango wa wanawake pamoja na kuwashirikisha katika ngazi za maamuzi.

“Tunawashuku wadau wote kwa kutuunga mkono kwa kutupatia bure mitungi ya gesi Oryx na majiko yake,meza pamoja na kreti 150 za Cocacola kwa ajili ya wanawake wajasiriamali wa Tanga.

“Tunaamini matumizi ya nishati ya gesi yatakwenda kumaliza matumizi ya kuni na mkaa katika kupikia.Nitoe rai kwa wanawake hiki ambacho tumekipata leo iwe ni chachu ya kuboresha biashara zetu,”amesema .

Aidha amewataka wajasiriamali hao wasijione wanyonge kwani wanaweza kufanya vizuri zaidi ya wanavyofanya sasa huku akifafanua kwa sasaa kuna watoto wengi wanamaliza vyuo na vyuo vikuu nafasi ya kuajiriwa ni chache.

“Kwa hiyo lazima tujiajiri na tuchukulie ujasiriamali kama ofisi rasmi, hivyo niendelee kuwaomba wanawake wajiamini na wajithamini katika kuimarisha biashara zenu.

“Serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan itaendelea kutambua na kuthamini mchango wa wanawake pamoja na kuwashirikisha wanawake katika nafasi za maamuzi.”

Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Oryx Gas Kanda ya Mashariki Shaban Fundi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benoit Araman ,amesema lengo la kutoa mitungi ya gesi ni kuendeleza kampeni yake ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia huku ikisisitiza pia Oryx gas imekua ikiyaishi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kwamba ifikapo 2032 asilimia ya 80 ya watanzania watumie nishati safi ya kupikia.

Shaban amesema matumizi ya gas yamekua yakiongezeka kwa kasi nchini kutokana na juhudi kubwa ya kuhamasisha inayofanywa na Oryx Gas kwa kushirikiana na wadau ikiwemo Serikali inayoongozwa na Rais Samia.

"Kwa ushirikiano mkubwa uliopo kati ya OryxGas na Cocacola, tumeendelea kuwezesha makundi mbalimbali ya wajasiriamali hususani wanawake maeneo mbalimbali nchini katika kuhamasisha watanzania wengi watumie nishati safi ya kupikia, " amesema.

Amefafanua kupika kwa Gas ya Oryx kunaimarisha afya kwa kuepuka kuvuta moshi mbaya wa kuni na mkaa,kupika kwa umaridadi na kwa wakati, hivyo kuongeza mapato mengi huku akikisitiza kwa ujumla ni pamoja na kulinda mazingira kwa kuzuia kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Ameongeza hivyo Oryx imeendelea kuwekeza kuhakikisha nishati hiyo inapatikana nchini kote lakini zaidi wanawekeza katika kutoa elimu kupitia makundi mbalimbali kuhusu matumizi sahihi ya Gas

Pamoja na hayo amesema kwa ushirikiano na Cocacola hadi sasa wamefanikiwa kutoa mitungi ya gesi ya Oryx zaidi ya 2000 na kuwafikia wajasiriamali 5000.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (kushoto) na Meneja Masoko wa Oryx Gas Kanda ya Mashariki Shaban Fundi (kulia) wakiwa wameshika mtungi wa gesi wenye ujazo wa kilo 15 kabla ya kukabidhi kwa mmoja ya wanawake wajasiriamali katika Jiji la Tanga



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...