Na Fauzia Mussa     Maelezo

Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar ZFDA  imeteketeza jumla ya tani 15 za vifaa tiba na vipodozi visivyofaa kwa matumizi ya Binaadamu.

Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo huko Kikungwi,Kaimu Mkurugenzi Idara  ya Dawa na Vipodozi  ZFDA  Haji Juma Khamis  amesema baadhi ya bidhaa katika mzigo huo zilipitwa na muda wa matumizi zikiwa sokoni na baadhi ziliingizwa Nchini Kinyume na utaratibu.

Alisema ZFDA ina jukumu la  kumlinda mtumiaji  hivyo mara tu wanapobaini bidhaa  zilizopoteza ubora huzuia na kuzifanyia uteketezaji bidhaa hizo endapo hakuna uwezekano wa kurudishwa zilikotoka.

Alifahamisha kuwa ZFDA  huteketeza vifaa tiba na vipodozi kwa kuzichoma moto kutokana na kukosa mashine maalum za kuangamizia bidhaa hizo kwa muda mfupi na kwa urahisi zaidi.

Hata hivyo Aliwashauri wafanyabiashara kuingiza  bidhaa kwa kuzingatia  muda wa kuishi na kuwataka kuagiza mzigo  kulingana na mahitaji ya soko ili kuepusha hasara zisizotarajiwa.

Vifaa tiba na vipodozi Vilivyopitwa na muda vikiteketezwa huko Kikungwi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

 Kaimu Mkurugenzi Idara  ya Dawa na Vipodozi  ZFDA  Haji Juma Khamis  akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na vifaa tiba na vipodozi vilivyoteketezwa kutokana na kutokufaa kwa matumizi ya binaadamu huko Kikungwi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...