

(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)
GEITA.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Emmanuel Tutuba, amesema kuwa jumla ya kilo 418 za Dhahabu tayari zimeshafirishwa kwenda nchini Uingereza kwaajili ya kuisajili kwenye soko la kimataifa na mfuko wa kuhifadhi dhamana na hifadhi za Kimataifa.
Gavana Tutuba amebainisha hayo leo Septemba 23, 2023 kwenye Mahojiano na Waandishi wa habari wakati wa ziara yake fupi ya kutembelea Banda la BoT kwenye Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya EPZ - Bomba mbili Mkoani Geita.
Amesema kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania toka ipate Uhuru, Serikali ilikuwa ikitunza fedha za kigeni ikiwemo Dola lakini sasa imeingia kwenye historia ya nchi zinazo hifadhi Dhahabu kutoka Tanzania.
"Tayari kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru tulikuwa tunatunza na kuhifadhi fedha za kigeni ikiwemo Dola, lakini kwa mara ya kwanza sasa imengia kwenye historia ya nchi zinazo hifadhi dhahabu ambayo imenunuliwa Tanzania,"amesema.
Ameeleza kuwa wamejipanga kuendelea kununua Dhahabu kwa wachimbaji wadogo, wakati na wakubwa, pamoja na wauzaji wengine waliopo kwenye maeneo mbalimbali, na kwamba wanaendelea kuhamasisha wananchi kutembelea banda la BoT kupata elimu na kufahamu namna ambavyo wanaweza wakauza dhahabu yao kupitia Benki hiyo.
"Hivi sasa kwenye Maonesho haya tunaendelea kuhamasisha watu waje kupata elimu na kufahamu namna ambavyo wanaweza wakauza dhahabu yao kupitia BOT.
"Kwasababu sisi tunanunua wenyewe, tunatoa bei halisi ya soko kwa siku hiyo, tofauti na wengine ambao wamekuwa wakinunua kwa bei za chini, inawezekana isiwape manufaa makubwa kama wanavyotarajia" ameeleza Gavana Tutuba,
Aidha amesema kuwepo kwao kwenye maonesho hayo kumetoa fursa kwa wananchi kufahamu mifumo yao ya kudhibiti uharifu kutokana na uwepo wa wachimbaji na baadhi ya wadau wa madini kupokea fedha nyingi au kutumia fedha tasilimu katika miamala yao ya kulipa au kupokea fedha hizo.
kutokana na changamoto hizo, BoT imetengeneza Mfumo wa kurahisisha unaoitwa 'Tanzania Payment System' (Tips). uliounganishwa mabenki yote na watoa huduma wa miamala kwa njia ya kampuni za simu.
"Kwa kutumia mfumo huu, umepunguza gharama za kuhamisha miamala kutoka Kampuni moja kwenda nyingine au kubadilishana kutoka benki moja kwenda nyingine" amesema Gavana Tutuba.









(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...