Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kutoa ufafanuzi wa tukio la kujiua kwa kujipiga risasi kwa aliyekuwa Askari J.2596 Konstebo wa Polisi Samwel Feston Kaziyote [24] wa kituo kikuu cha Polisi Mbeya.
Ni kwamba, Oktoba 02, 2023 majira ya saa 2:15 usiku huko maeneo ya Mtaa wa Mzumbe Forest ya zamani, Jijini Mbeya Askari huyo alijipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake papo hapo.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea baina yake na mpenzi wake baada ya marehemu kuacha lindo la Benki na kisha kuondoka na silaha bunduki kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo na kujipiga risasi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...