*Aagiza mabasi 70 yaendayo haraka yatengenezwe haraka.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanategemea huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka na kuwataka watoa huduma ya usafiri ya mabasi hayo kutoa huduma bora pasipo kuacha msongamano kwenye vituo.

Chalamila ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kuangalia huduma huduma ya usafiri kuanzia majira ya saa 12 Asubuhi kuanzia Jangwani hadi Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.

Amesema kuna mabasi 70 ni mabovu na kutaka mtoa huduma UDART kutengeneza na kama akishindwa kufanya hivyo kutafuta suluhu ambayo itasaidia wananchi kupata huduma.

Chalamila amesema Serikali ya awamu ya sita ipo katika kuhudumia wananchi hivyo kama wasaidizi sio sehemu ya kumuangusha Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Chalamila amesema kuwa katika ziara hiyo amejifunza kitu ambapo leo wametoa mabasi yote na kuonekana wananchi kupata huduma hiyo na kuahidi kuweka kambi katika vituo hivyo kwa kificho ili kujiridhisha kwa vilio vya wananchi.

Aidha amesema jambo la wananchi kukaa vituoni kwa muda wa masaa mawili ni jambo linalochelewesha uchumi na kufanya suala la usafiri mabasi yaendayo haraka kuwa sehemu ya changamoto hivyo wakati umefika UDART kutoa malalamiko dhidi ya serikali.

Hata hivyo amesema kuwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka na miundombinu yake bado inajengwa katika nia ile ile ya serikali kurahisisha huduma ya usafiri mijini.

Mkazi wa Mbezi Joseph Masawe amesema usafiri wa mabasi yaendayo haraka ni changamoto na kutaka kuwa na ushindani wa utoaji wa huduma hiyo.

Masawe amesema kuwa serikali iangalie huduma usafiri kuwasaidia wananchi katika usafiri huo na kushukuru.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza na wanafunzi wakati alipotembelea huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka  katika kituo  cha mabasi yaendayo haraka Kimara.
 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akimsikiliza mchungaji Machimo wakati alipotembelea kituo cha mbezi Luis kuangalia huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka
 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akiwa katika Basi yaendayo haraka wakati akiangalia huduma ya mabasi hayo.
 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akimsikiliza mwananchi  katika kituo cha Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...