"ha"
Showing posts with label ha. Show all posts
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe profesa Adolf Mkenda amesema serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika Wilaya 64 nchini.

Waziri Mkenda amesema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka minne.

Waziri Mkenda amesema kuwa ujenzi wa vyuo hivyo ni utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kuhakikisha vijana wengi zaidi wanapata fursa za mafunzo ya Ufundi Stadi.

Waziri Mkenda amesema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliagiza fedha zitolewe ili kukamilisha ujenzi wa vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ambavyo hazijakamilika ili zianze kufanya kazi haraka.

Amesema kuwa kwa Tanzania Bara kila mkoa utakuwa na VETA yenye hadhi ya mkoa hivyo kazi ya Wizara yake ni kuzitengeneza hizo VETA ili ziweze kutoa watu ambao wana ujuzi na uwezo wa kufanya kazi ndani na nje ya nchi.

 


KAMPUNI namba moja ya michezo ya kubashiri nchini Betika imezindua rasmi Kampeni yake kubwa ya "Mtoko wa Kibingwa " kwa Msimu wa 7 kwa wateja wake na kuendelea kutimiza ndoto za mashabiki wa soka.

Akizungumza na Wanahabari Februari 19, 2024 Afisa Habari wa Betika Rugambwa Juvenalius amesema Kampeni hiyo imezinduliwa Leo ambapo droo zitaanza Februari 27,2024 hadi kufikia tamati Aprili 10,2024 na Mabingwa 56 kushuhudia derby ya watani wa Jadi kati ya Simba na Yanga katika Jukwaa la VIP A.

Aidha Juvenalius ameeleza sababu ya kuwepo kwa Kampeni hiyo ina lenga kuwaleta pamoja mashabiki wa soka na kuwapa fursa ya kufurahia burudani ya kipekee ya kushuhudia mechi ya watani wa jadi bila longolongo.
"Kampuni yetu ya Betika katika mtoko huu wa Kibingwa itahakikisha inatoq zawadi za wiki,za mwezi pamoja na Usafiri wa Tiketi za Ndege kwa washindi watakaopatikana Mikoani na gharama za kila kitu zitalipwa na sisi wenyewe betika ."

Pia amesema kampeni hiyo inamuhitaji mshiriki abashiri kwa mikeka mitatu ambapo dau lake ni shilingi elfu 2 tu.
"Mshiriki atatakiwa kuweka ubashiri kwa dau la 2,000 mechi zaidi ya 3 anaingia kwenye droo ya ushindi ".

"Hata hivyo watakaobashiri mara nyingi zaidi kwa wiki na kutofanikiwa kushinda mikeka hiyo watapata zawadi ya simu Android wakati watakaobashiri zaidi kwa mwezi watajishindia simu aina ya Iphone 15.

"Kumbuka mkeka utiki au usitiki unaingia kwenye droo ya kushinda mtoko wa kibingwa hivyo waendelee kuweka ubashiri wao kupitia www.betika.co.tz au piga *149*16#.

*Aagiza mabasi 70 yaendayo haraka yatengenezwe haraka.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanategemea huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka na kuwataka watoa huduma ya usafiri ya mabasi hayo kutoa huduma bora pasipo kuacha msongamano kwenye vituo.

Chalamila ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kuangalia huduma huduma ya usafiri kuanzia majira ya saa 12 Asubuhi kuanzia Jangwani hadi Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.

Amesema kuna mabasi 70 ni mabovu na kutaka mtoa huduma UDART kutengeneza na kama akishindwa kufanya hivyo kutafuta suluhu ambayo itasaidia wananchi kupata huduma.

Chalamila amesema Serikali ya awamu ya sita ipo katika kuhudumia wananchi hivyo kama wasaidizi sio sehemu ya kumuangusha Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Chalamila amesema kuwa katika ziara hiyo amejifunza kitu ambapo leo wametoa mabasi yote na kuonekana wananchi kupata huduma hiyo na kuahidi kuweka kambi katika vituo hivyo kwa kificho ili kujiridhisha kwa vilio vya wananchi.

Aidha amesema jambo la wananchi kukaa vituoni kwa muda wa masaa mawili ni jambo linalochelewesha uchumi na kufanya suala la usafiri mabasi yaendayo haraka kuwa sehemu ya changamoto hivyo wakati umefika UDART kutoa malalamiko dhidi ya serikali.

Hata hivyo amesema kuwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka na miundombinu yake bado inajengwa katika nia ile ile ya serikali kurahisisha huduma ya usafiri mijini.

Mkazi wa Mbezi Joseph Masawe amesema usafiri wa mabasi yaendayo haraka ni changamoto na kutaka kuwa na ushindani wa utoaji wa huduma hiyo.

Masawe amesema kuwa serikali iangalie huduma usafiri kuwasaidia wananchi katika usafiri huo na kushukuru.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza na wanafunzi wakati alipotembelea huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka  katika kituo  cha mabasi yaendayo haraka Kimara.
 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akimsikiliza mchungaji Machimo wakati alipotembelea kituo cha mbezi Luis kuangalia huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka
 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akiwa katika Basi yaendayo haraka wakati akiangalia huduma ya mabasi hayo.
 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akimsikiliza mwananchi  katika kituo cha Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam.