Raisa Said,Tanga
Walimu wameaswa wasiwe sababu ya watoto kukatisha ndoto zao kwa kuwakatisha tamaa juu ya masomo wanayotakiwa kuyachukua kufikia ndoto hizo.
Wito huo umetolewa na Meya wa Jiji la Tanga, Abdulrahaman Shiloo alipokuwa akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani yaliyofanyika Jijini Tanga.
“Walimu mnaweza kuharibu ndoto. Kama mtu anataka kuchukua masomo fulani ambayo yatamfikisha katika ndoto zake mnatikiwa muwasaidie sio kuwakatisha tamaa,” alisisitiza.
Akizungumzia kilio cha maslahi duni ambacho walimu wamekuwa akikipigia kelele, Shiloo alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa kazi ya ualimu kwa sababu katika kulitengeneza taifa.
“Ualimu ni kazi ya kwanza. Kazi ya kwanza kwa Mungu alifanya kwa Adamu ni ya ualimu, kumfundisha vitu vyote vilvyopo alivyoviumba ka majina,” alisema Shiloo.
Alisisitiza kuwa walimua wanafanya kazi bora kwa sababu hakuna kiumbe mwanadamu ambaye hakupita kwa mwalimu. “ Lazima mjivunia kazi yenu,”alisema.
Alisema kuwa serikali inawakumbuka pamoja na umaskini. Akawahakikishia kuwa kuhsu maslahi kuwa itafika mahali yataboreshwa kwa kutambua umhimu wao.
“Itafika mahali maslahi ya walimu yataboreshwa. Najua mnaona kuwa ni ndoto. Ni suala la watu kubadili mitazamo. Ujerumani mwalimu ndiye anayelipwa mshahara mkubwa. Na hapa itafika siku,” alisema.
Walimu wlaiohudhuria tamasha hilo walito maoni yao wakizuungumzia changamoto mbalimbali ikiwenmo suala ya maslahi duni.
Akitoa maoni yake, mwalimu Tatu Omari alisema kuwa serikaliiwaangalie walimu kuinua kiwango cha mshahara na maslahi. “Tunaishimaisha ya tabu kama unavyojua hatuna posho. Zamanikulikuwa na posho ya kufundisha. Sasa vhivi hakuna,” alillalamika.
Naye Mwalimu Omari Gumbo Yasini wa Shule ya Msingi Mapakani, Tanga alizungumzia sula a la kikotoo ambalo alisema ni kilio cha wengi.
“Serikali itazame kwa makini kwa sababu watu wengi wanafika mahala wanaona kazi hii ni adha. Warejeshe malipo ya gharama za benki na uafirishaji.
Vitu ambavyo pengine vitatuwezesha tuishi vizuri baadaa ya kustaafu,” alisema Mwalimu Yasini ambaye alieleza kuwa anakaribia kustaafu..
Katibu wa CWT Jiji, Godfrey Rumba, alisema kwa kuwa siku ya Mwalimu Duniani ina madhumuni ya kutambua juhudi kubwa za walimu kuelimisha taifa, serikali itambue walimu wanafanya wajibu gani kwa taifa na kuwapa stahili zao kwa uzito unaostahili.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Walimu, Taifa, FarajiAli Juma, alisema kuwa suala la kikotoo liko mezani likiwa linafanyiwa kazi.
Meya wa Jiji la Tanga Abdul Rahman ShilooKatibu wa Chama Cha Walimu (CWT) Jiji la Tanga Godfrey Rumba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...