Raisa Said ,Tanga

Mkoa wa Tanga Umezindua rasmi Mpango Jumuishi wa Taifa wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya  awali ya Mtoto (PJT_MMMAM) ambapo  Wazazi wametakiwa kuuunga mkono mpango huo ili kuboresha kiwango kisichorishidhisha cha watoto wenye umri kati ya miaka 0 hadi 8 ambao hawajafikia ukuaji timilifu.

Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Kanali Maulid Hassan Sarumbu, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba alizindua mpango huo kwa melekezo kwa  maafisa wa serikali, viongozi na taasisi kuhakikishat uekelezaji wake unafanyika kwa ufanisi.

“Ili kufikia matarajio ya watoto wa Kitanzania, wazazi na sekta binafsi wawekeze katika maendeleo ya watoto wadogo kuanzia mwaka 0 hadi miaka name" Alisema

Kwa mujibu wa Joel Mwakapala, mwakilishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii (Programu Maalum), programu hii, iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan mwaka 2021, ina malengo ya kuwapa watoto wenye umri kati ya miaka 0 na 8 uwezo kufikia ukuaji timilfu.

Alisisitiza umuhimu wa ahadi hii, akihakikisha kwamba kila mtoto anaongozwa kuelekea wakati ujao mzuri, na kukuza kimamaendeleo.

Mwakapala alisisitiza kuwa Rais anatambua umuhimu wa watoto kama rasilimali muhimu ya taifa. Rais alisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika malezi ya awali na maendeleo ya watoto,  akisema kuwa sio faida tu ya watoto wenyewe bali pia ni kwa taifa zima.

Alisema mpango huo kwa sasa unazinduliwa katika mikoa 16, ikiwamo Tanga. Mikoa  10 ilikwisha zindua mpango huo. 

Kwa mujibu wa Dk. Regis Temba, Mkurugenzi  wa taasisi isiyo ya  kiserikali ya  UHTC alieleza kuwa  asilimia ya watoto wenye umri kati ya miaka

sifuri hadi miaka 8 katika mkoa wa Tanga ambao wamefikia ukuaji timilifu ni 46.

Wakati wa mahojiano baada ya Mpango kuzinduliwa rasmi, Dk. Temba alisisitiza kuwa asilimia 53 ya watoto katika mkoa huo bado Hawajafikia utimilifu wa ukuaji.

Alisisitiza kuwa hatua ya utotoni ina ushawishi mkubwa sana katika maisha ya mtoto. Alidokeza kwamba ikiwa kuna upungufu wowote katika

maendeleo yao wakati huu muhimu, inaweza kuwa na matokeo ya muda mrefu ambayo hatimaye huzuia nafasi zao za kufikia uwezo wao kamili katika maisha ya baadaye Alisema mpango huo unalenga kuimarisha na kuinua kiwango cha maendeleo  na makuzi ya watoto wachanga katika mkoa huo.





.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...