*Kuanza Oktoba 21 vituo mbadala vyatajwa

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imetoa vituo mbadala kwa basi zilizokuwa zikitumia Kituo cha Kivuko Feri.

Hatua ya kutotumia kituo cha kivukoni ni kutokana na kituo hicho kuanza matengenezo kwa ajili ya miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo hataka awamu ya Nne.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano DART  William Gatambi amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho utaanza hivi karibuni hivyo Oktoba 21 kutakuwa na utepe ambapo Daladala hazitaingi kupakia wala kushusha abiria katika kituo hicho.

Amesema vituo mbadala ni kituo cha Ardhi kwa mabasi , Kituo cha Uhio na Baharini NBC kwa dalada zilizopangiwa kutokana na barabara zinazotumia.

Gatambi amesema upanuzi wa kituo cha Kivukoni kitatumiwa na mabasi yaendayo haraka pale kitapokamilika daladala hazitaingia.

Afisa Mfawidhi wa LATRA jiji la Dar es Salaam Rahim Kondo amesema kuwa daladala zote zifike katika vituo vilivyopangwa na bila kufanya hivyo watakuwa wamekiuka taratibu za leseni.

Amesema kuwa baadhi ya madereva wa daladala wataanza kushusha sehemu ambazo hawajapangiwa kwa madai ya kuwa hawatakiwi kufika.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam Shufwaya Lema amesema wanakubaliana na maendeleo na kwenda kuwapa taarifa madereva wa Daladala .

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa  Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) William Gatambi akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ujenzi awamu ya Nne unahusisha ujenzi wa Kituo cha Kivukoni ambapo katika ujenzi huo Daladala na huduma zingine za usafiri zingine hazitafanya kuwa sehemu ya abiria , jijini Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wamiliki wa Daladala Jiji la Dar es Salaam Shufwaya Lema akizungumza kupokea taarifa hiyo kwa kwenda kutekeleza kwa madereva kutotumia kituo cha kivukoni , Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...