Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the IMF– for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada, mjini Marrakech, nchini Morocco, ambapo Tanzania imeeleza kuhusu kuimarika kwa uchumi wa nchi, katika Nusu ya Kwanza ya Mwaka (Januari hadi Juni, 2023), uchumi umekua kwa asilimia 5.3, ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (katikati), ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the IMF– for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Willie Nakunyada (wa tatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo mjini Marrakech, nchini Morocco, ambapo Tanzania imeeleza kuhusu kuimarika kwa uchumi wa nchi, katika Nusu ya Kwanza ya Mwaka (Januari hadi Juni, 2023), uchumi umekua kwa asilimia 5.3, ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wa tatu kulia), Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban (wa pili kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (wa pili kushoto) na Kamishna Msaidizi, Idara ya Sera kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Mbayani Saruni.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – WF, Marrakech, Morocco)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...