Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya utengenezaji wa mifumo katika sekta ya Afya (GPITG) Aderld Kiliba akizungumza na Michuzi blog/Michuzi TV leo Oktob 4, 2023, wakati wa mkutano wa kumi wa wadau wa Afya Tanzania ( THS) unaoendelea kufanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere(JINCC) jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya utengenezaji wa mifumo katika sekta ya afya ya GPITG, imesema wako katika hatua za mwisho kukamilisha mfumo wa kusaidia upatikanaji wa taarifa za mgonjwa kutoka hospitali moja kwenda nyingine.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Adelrd Kiliba amewahakikishia Watanzania kwamba mara mfumo huo utakapoanza kutumika, kutakuwa na usiri na kwamba mgonjwa ndiye mwenye mamlaka ya kutaka taarifa zake zipeleke hospitali nyingine au la.
Kiliba amesema "mgonjwa atakayepatiwa matibabu katika hospitali za chini na kupewa rufaa, taarifa zake zitapelekwa moja kwa moja katika hospitali hiyo hivyo kusaidia upatikanaji wa taarifa."
Amesisitiza kuwa kwa kutumia mfumo huo wataongeza ufanisi wa utoaji huduma za afya.
Amesema wako katika hatua za mwisho za kukamilisha mfumo huo na kwamba tayari wamefanya majaribio katika hospitali mbalimbali mkoani Kilimanjaro.
Amesema wanatarajia baada ya mfumo huo kutoa matokeo, uweze kutumika nchi nzima.
"Tunawahakikishia watanzania kuwa teknolojia hii itakapotumika kuongeza usiri katika taarifa zake na ni pale mgonjwa atakapotaka taarifa zake zitumike kutoka hospitali moja kwenda nyingine," amesisitiza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...