Na.Vero Ignatus,Arusha
Tanzania inatazamia kuwa mwenyeji wa kikao cha 77 cha kawaida cha cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, kinachotarajiwa kufanyika Jijini Arusha katika kumbi za AICC kuanzia tarehe 20 Oktoba mpaka tarehe 9 Novemba mwaka huu,ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Balozi Dkt.Pindi Chana amewaambia waandishi wa habari Jijiji Arusha kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Serikali inaendelea na maandalizi ya kikao chacho,ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa yakiwemo Taarifa ya haki za binadamu Afrika, Taarifa za nchi mbalimbali za haki za binadamu, wuwezeshaji wa wanawake Tanzania pamoja na Hali ya Watu wanaoishi na VVU Barani Afrika.
Aidha Waziri Dkt Chana amesema kuwa mbali na wageni hao mikutano ya Kimataifa inayofanyika hapa nchini ni fursa ya kutangaza lugha adhimu ya Kiswahili ambayo ni mojawapo ya Lugha Rasmi ya Kikazi ya Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Jumuiya kadhaa za Kikanda Barani Afrika.
Akielezea hatua ya maandalizi ya Kikao hicho mbele ya Makatibu Wakuu kutoka Wizara zilizoalikwa na viongozi wengine wa Taasisi Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo alisema hatua za maandalizi ya kikao hicho kinachotarajiwa kuwa na watu wasiopungua 700 yanaendelea vyema hasa kutokana na ushirikiano unaotolewa Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Fedha iliyopitisha fedha kwa ajili ya kikao hicho.
Aidha, Katibu Mkuu aliwaomba viongozi na watumishi waliohudhuria kikao hicho cha maandalizi kupitia taarifa ya kamati ya maandalizi kuiboresha ili iweze kuwasilishwa kwenye kikao cha Mawaziri na hatimaye kwa pamoja taifa liweze kufakinisha kikao hicho na kuleta tija kwa watanzania na waafrika kwa ujumla.
"Tutapata fursa ya kujadiliana katika masuala ya haki za binadamu na watu fursa za kijamii pamoja na zile za kiuchumi huku sekta mbali mbali Maliasili na Utalii habari na mawasiliano utamaduni na Sanaa ambapo tunategemea wageni zaidi ya 700 kutoka Mataifa mbalimbali barani Afrika"Alisema Makondo
Aidha Kamisheni hiyo inapaswa kutekeleza majukumu makuu 3 ikiwemo Ulinzi wa haki za binadamu na watu,Kukuza haki za binadamu na watu pamoja na kutoa tafsiri ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na watu
Sambamba na hayo mkutano huo utahusisha sekta mbalimbali zaidi ya sekta ya sheria na haki za binadamu na watu kama vile maliasili na utalii,ushirikiano wa kimataifa ,utamaduni sanaa na michezo,uchumi na fedha ,ulinzi na usalama afya na habari na mawasiliano.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhia mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na watu tarehe 18 februari 1984 ambapo mkataba huo umeanzisha kamisheni ya Haki za binadamu na watu,ambapo ilizinduliwa 2novemba 1987 huko Addis Ababa Ethiopia na sekretarieti ya kamisheni hiyo ipo Banjui Gambia
Adha Ridhaa ya mwitikio wa Serikali ya Tanzania iliwasilishwa rasmi kwenye Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu pamoja na Umoja wa Afrika (AU) wakati wa mkutano wa Wakuu wa Nchi Februari, 2023,hivyo iliwasilisha maombi yake rasmi kwa Serikali kuandaa kikao tajwa kuanzia tarehe 20 Oktoba hadi 9 Novemba, 2023.
Home
HABARI
KIKAO CHA 77 CHA TUME YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU KUFANYIKA ARUSHA 20OCT -9NOV,2023
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...