SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu imebainisha kuwa itaendelea kushirikiana na nchi ya Norway kwa kuunganisha watafiti wa nchi hizo ili kubadilishana uzoefu na hivyo kuwezesha ufanyikaji wa tafiti zenye ufanisi na tija katika mendeleo ya taifa


Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ambapo amesema kuwa kwa sasa nchi hizo zinatekeleza Miradi 18 ndani ya vyuo 9 tofauti nchini lengo likiwa ni kujaidil na kuona namna bora ya kuendelea na tafiti hizo

Kwa upande wake Kaimu Naibu Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam anayeshughulika na masuala ya Utafiti prof. Nelson Boniface amesema baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kupitia miradi hiyo kuwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya kufundishia na kufanya tafiti sambamba na kutoa wataalamu wenye umahiri katika ufanyaji wa tafiti


Naye Balozi wa Norway nchini Tanzania amesema kuwa lengo ni kujifunza zaidi juu ya ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili na kusisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na wataalamu mbalimbali kutoka nchini ili kuwezesha ufanyikaji wa tafiti zenye tija katika maendeleo ya jamii.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...