Na Ramadhani Kissimba, WF, Kyela
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwasili katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilizopo katika mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu Wilayani Kyela, mkoani Mbeya. Kushoto kwake ni Meneja Msaidizi wa Fordha kutoka Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya, Bw. Nsajigwa Mwambegele.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akifuatilia Mkutano wa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ((Mb), uliofanyika Wilayani Kyela mkoani Mbeya. Kulia kwa Bw. Mwandumbya ni Naibu Kamishina Mkuu kutoka Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha na anayefuatia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela, Mhe. Ally Mlagila Jumbe.Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiongea na wananchi wa Kitongoji cha Kilambo, Kata ya Njisi, Wilani Kyela (Hawapo pichani) mara baada ya kutembelea na kukagua shughuli za kiuchumi na maendeleo katika mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu, mkoani Mbeya. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kyela,Bw. Elias Mwanjala.Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akisani kitabu cha wageni katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilizopo katika mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu Wilayani Kyela, mkoani Mbeya.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) akifurahia jambo wakati wa Mkutano na wananchi wa Kitongoji cha Kilambo, Kata ya Njisi Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya. Kushoto kwa Mhe. Dkt. Nchemba ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kyela Bw. Elias Mwanjala na kulia ni Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) na anayefuatia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF, Kyela)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...