Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 3 Oktoba, 2023 amewasili Accra nchini Ghana na kupokelewa na mwenyeji wake Spika wa Bunge la nchi hiyo Mhe. Alban Bagbin.
Dkt. Tulia anatarajia
kushiriki Mkutano wa 66 wa Kibunge wa Jumuiya ya Madola (CPC) utaofanyika
nchini humo kuanzia tarehe 3-6 Oktoba, 2023 yenye dhima isemayo “Miaka 10 ya
Mkataba wa Jumuiya ya Madola: Maadili na Kanuni za kuzingatiwa na Mabunge”
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na kuzungumza na Spika
wa Bunge la Ghana Mhe. Alban Bagbin wakati alipowasili katika Jiji la Accra,
Ghana ambapo anatarajia kushiriki Mkutano wa 66 wa Kibunge wa Jumuiya ya Madola
(CPC) utaofanyika nchini humo kuanzia tarehe 3-6 Oktoba, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...