Na. Edmund Salaho/Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna wa Polisi, Benedict Wakulyamba leo, tarehe 04.12.2023 ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo ya ukarimu kwa wateja kuongeza ufanisi zaidi katika kutoa huduma kwa wateja katika maeneo yote ya Hifadhi za Taifa nchini.
Kamishna Wakulyamba, ametoa rai hiyo leo jijini, Dodoma wakati akifunga mafunzo ya huduma bora kwa wateja kwa watumishi waliopo katika mstari wa mbele katika kutoa huduma kwa wateja kwenye maeneo yote ya utalii (front line staff) katika Hifadhi za Taifa mafunzo ambayo yametolewa kwa siku 3 kuanzia tarehe 02.10.2023 hadi tarehe 04.10.2023.
“Ili kuendeleza sekta ya utalii nchini na vivutio vyake ni muhimu kuhakikisha kuwa watumishi waliopo katika mstari wa mbele katika kutoa huduma kwa wateja kwenye maeneo yote ya utalii (front line staff) wanapata mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutoa huduma kwa viwango vitakavyowaridhisha wateja hao.
Ni matarajio yangu kuwa mafunzo haya mliyoyapata kutoka kwa wataalam wetu yatawajengea uwezo wa kutosha kutoa huduma bora na kufikia matarajio yanayokusudiwa.” alisema Kamishna Wakulyamba.
Pia, Kamishna Wakulyamba aliwataka washiriki wote waliopata mafunzo hayo kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anatoa huduma bora na kuunga mkono jitahada za Serikali katika kukuza utali nchini.
“Nawaagiza wote mliopata mafunzo haya mnaporudi katika vituo vyenu vya kazi muwe mfano bora kwa kutoa huduma kwa wateja ili tufikie viwango vya hali ya juu na hivyo kupeleka chachu ya mabadiliko chanya katika Tasnia ya utalii hapa nchini”
Awali, Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara -TANAPA, Herman Batiho alibainisha kuwa mafunzo haya yamewaongezea mbinu za kuwahudumia wateja kwa umakini na kusikiliza mahitaji yao .
“Ni dhahiri kuwa mafunzo haya mliyoyapata yamewaongezea mbinu za kuwadumia wateja. Watalii wetu wakipata huduma bora ni rahisi kuridhika na huduma waliyopatiwa na hatimaye kuwa mabalozi wazuri wa kuwavuta na wateja wengine kutembelea hifadhi za taifa nchini.”
Aidha, Kamishna Batiho aliupongeza uongozi wa Benki ya Azania kwa kujitoa kwao kufadhili mafunzo hayo, halikadhalika uongozi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) kwa kuratibu mafunzo hayo ambayo ni dhahiri kuwa yataleta mabadiliko chanya wakati wa kuhudumia watalii ndani ya Shirika letu.
Pia, Batiho alibainisha kuwa Shirika kwa sasa linatekeleza shughuli zake kwa viwango vya kimataifa (ISO 9001:2015) ambapo moja ya nguzo muhimu ya kiwango hicho cha ubora ni kutoa huduma iliyo bora kwa wateja. Hivyo, mafunzo hay ni mwendelezo wa utekelezaji wa viwango hivyo vya ubora wa kimataifa.
Kwa upande wake Charles Mugilla, ambaye ni Mkurugenzi wa sheria kutoka Benki ya Azania, aliahidi ushirikiano zaidi na kuongeza kuwa benki ya Azania iko tayari kushirikiana na wizara na taasisi zake muda wote watakopo wahitaji.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Elifas Bisanda aliwashukuru TANAPA kwa kutoa fursa kwa chuo hicho ili kutoa uzoefu wao katika maswala mbalimbali ya kitaaluma.
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja baadhi ya maafisa na askari wapatao 100 kutoka kada mbalimbali ambao wapo katika mnyororo mzima wa utalii ndani ya TANAPA wamepatiwa Mafunzo ya utoaji huduma bora kwa wageni.
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...