Mwandishi wetu
SHIRIKISHO la Sanaa za Ufundi na Ubunifu limesema Serikali ina mikakati ya kupeleka wabunifu nje ya nchi kwa lengo la kukuza uchumi na kuleta fedha za kigeni nchini.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Rais wa BASATA Adrian Nyangamale, wakati akiongea na wabunifu wa mitindo ambapo aliwataka wabunifu kuongeza ubunifu wa kazi zao ili masoko yao yakatangazwe katika soko la Dunia .
Akizungumzia siku ya uzinduzi wa usiku wa ubunifu wa mitindo ya mavazi iliyoandaliwa na Taasisi ya Collection Fashion Academy (AFA) alisema BASATA inatambua mchango unaotolewa na tasnia ya ubunifu nchini.
Alisema kuanzishwa kwa chuo hicho ni msaada mkubwa kwa wabunifu wanaotumia cherehani.
“AFA imekwenda kuwaheshimisha mafundi cherehani kwa sababu watajitahidi kufanya ubunifu mzuri ili bidhaa zao wanazozitengeneza zikashindaniwe katika soko la dunia”,alisema Nyangamale.
Alisema Tanzania ipo katika uchumi wa kati ambapo watu wake wana fedha na mtu mwenye fedha anapenda kuvaa vizuri hivyo wabunifu waendelee kubuni kwa lengo la kupata fedha na kutangaza masoko yao ndani na nje ya Nchi.
Aidha, alisema kuwa yeye binafsi angependa wanafunzi wanaosoma katika Chuo hicho cha AFA wakitoka hapo wasiwe mafundi wa kawaida ila wawe wabunifu wakubwa wa mitindo.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa chuo hicho Anna Lungoya alisema lengo la kuanzisha chuo hicho ni kukuza sanaa za ubunifu.
Alisema hadi sasa chuo hicho kinawanafunzi 300 waliotoka ndani na nje ya nchi .
Mkurugenzi huyo alisema hivi sasa wameanzisha jukwaa la pamoja kwa lengo la kuonyesha bunifu za wanafunzi linaloitwa Anna Collection Fashion Academy (AFA).
“Siku nyingi nilikuwa najiuliza hawa wanafunzi tunawapa elimu ya mitindo ya bunifu lakini je baada ya hapo watazipeleka wapi bunifu zao kwani ukimfundisha mwanafunzi alafu ukamuacha aende zake unakuwa hujamsaidia”,alisema.
"Nikapata jibu kuwa nina umuhimu wa kuanzisha jukwaa ambalo hilo kazi yake litakuwa ni kuboresha bunifu nyingi zilizofanywa na wanafunzi hao kwa lengo la kupata masoko ndani na nje ya nchi na badaye kujipatia kipato,”alisema Anna
Alisema Novemba 26 mwaka huu,wanafunzi wake wataonyesha bunifu zao kwa lengo la kujitangaza sehemu mbalimbali.
Pia, Balozi wa AFA Jacqueline Wolper alisema amefurahi kuwa balozi wa chuo hicho na atahakikisha anakifikisha mbali katika jitihada zao za ubunifu.
“Hawa wabunifu wa mitindo na wao wanatakiwa wafahamike na michango yao ionekane ndani ya Taifa letu na Nje ya Nchi hivyo basi hivi sasa fani hii imeheshimishwa kwa kiasi kikubwa na AFA kwa hiyo hata sisi inabidi tuunge mkono katika kuhakikisha wanasonga mbele zaidi,”alisema Wolper.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...