Kamishna  Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Baraka Makona akiwa katika picha ya pamoja na Wamiliki wa Vituo vya Kulelea Watoto Mchana, Walezi wa Vituo vya kulelea watoto Mchana mara baada ya kufungua kufungua mafunzo ya siku sita  leo Oktoba 2023, jijini Dar es Salaa.
Kamishna  Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Baraka Makona akizungumza wakati wakufungua mafunzo ya siku sita  leo Oktoba 2023, jijini Dar es Salaa wakati wa kufungua mafunzo ya siku sita kwa maafisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Wamiliki wa Vituo vya Kulelea Watoto Mchana, Walezi wa Vituo vya kulelea watoto Mchana.

Na Avila Kakingo, Michuzi TV
KATIKA Kuhakikisha Watoto wanakuwa salama, Shirika la Children in Crossfire(CIC) kupitia Mradi wa Programu jumuishi ya malezi na makuzi na maendeleo Awali ya mtoto kuanzia umri wa miaka 0-8 (PJT-MMMAM) wametoa elimu kwa maafisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Wamiliki wa Vituo vya Kulelea Watoto Mchana, Walezi wa Vituo vya kulelea watoto Mchana.

Akizungumza wakati wakufungua mafunzo ya siku sita  leo Oktoba 2023, jijini Dar es Salaa, Kamishna  Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Baraka Makona, amesema kuwa jitihada hizo zinafanyika katika kuhakikisha watoto wanakuwa Salama kwasababu Changamoto bado zipo za masuala ya ukatili dhidi ya watoto. 

Amesema kwenye maeneo ya mjini hasa Jijini la Dar es Salaam ambao shughuli nyingi zakiuchumi zinazosababisha wazazi wasikae na watoto wao kwa muda mrefu.

Amesema katika mkoa wa Dar es Salaam kuna vituo vya kulelea  watoto mchana zaidi ya 3,000 kwahiyo jicho la pekee linatakiwa litokee katika mkoa wa huo ambapo watu wapo kila siku katika harakati za kiuchumi ili kuchangia pato la taifa. 

"Watu wote wa watoto, sasa wanawapeleka wapi? na upo kazini, lazima kuwe na mbadala wa kuwasaidia." Amesema Makona

Pia anesema namna ya kuwasaidia akinamama wanaotembea na watoto wao masokoni wakiuza bidhaa mbalimbali na kuchangia pato la taifa pia watoto wasikose malezi, ndio maana serikali inashirikiana na taasisi binafsi ili kuhakikisha tunachangia katika programu kubwa za kitaifa za kuhakikisha wananchi wanakuwa na muda wa kuongeza uzalishaji.

Makona amesema kuwa vituo hivyo vimeanzishwa na kusajiliwa iliviweze kusaidia na nilazima viwe na walezi bora watakao kuwawaangalia watoto kwakipindi cha masaa 12 ya mchana ambayo watoto wanashinda pale. 

Pia amesema vituo hivyo haviruhisiwi kwa mujibu wa sheria kuweka au kulea watoto usiku. 

Akizungumzia faida za kuwapeleka watoto kweye vituo vya malezi na makuzi Makona amesema kuwa watoto watapata viungo mhimu vitano ambavyo vipo kwenye programu jumuishi vinatekelezwa ambavyo ni kuzingatia afya ya mtoto, Ulinzi na usalama, lishe na malezi kwawatoto ambao watashinda kwenye kituo. 

Kwa upande wa kaimu Mkurugenzi Chidren Crossfire (CIC), Heri Ayubu  amesema malengo makuu ni kuangalia sekta nyeti ambayo inajihusisha na malezi, Ulinzi makuzi na maendelo ya watoto.

Amesema sehemu ambayo inaangalia watoto hasa kwa wenye umri chini ya miaka nane ni vituo vya kulelea watoto mchana wakiwa wajibu wa kulea watoto walio chini ya miaka mitano kati ya miaka miwili na miaka wanaoachwa katika vituo hivyo. 

"Walezi wa vituo wanapokuwa hawana ujuzi namna gani ya kufanya na masuala ya kuzingatia, kanuni nasheria za nchi masuala ya kiusalama ni hatarishi kwa watoto, lakini kitaifa watoto ndio rasilimali watu ya taifa kwahiyo vituo vinaowajibu wakuwaandaa watoto kwenye elimu ya awali na kazi mojawapo ni kuweka mazingira ya watoto kufikia uwezo wa kujiunga na darasa la awali wakiwa na utimilifu." Amesema

Amesema katika vituo hivyo kuna kazi ya elimu ya awali ikiwa sambamba na elimu ya malezi kwa watoto. 

Pia amesema baada ya mafunzo hayo ya siku sita wataangalia namna bora ya kufikia vituo vingi zaidi ya waliopewa  mafunzo ya malezi na Makuzi ya awali kwa watoto katika vituo vyao.

Picha za pamoja.




Baadhi ya wadau wa malezi na makuzi ya watoto wakizungumza wakati wakufungua mafunzo ya siku sita  leo Oktoba 2023, jijini Dar es Salaa






Baadhi ya washiriki wakiwa katika wakufungua mafunzo ya siku sita  leo Oktoba 2023, jijini Dar es Salaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...