Na Janeth Raphael - MichuziTv

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau imekuja na mfumo wa kuweka vifaa vya teknolojia ya mawasiliano kwa kupokea na kuchambua mwenendo wa majanga nchini.

Mhe. Nderiananga ameyabainisha hayo leo Oktoba 13,2023 Jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa inayoenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Imarisha usawa kwa uthabiti endelevu.

Aidha amesema kuwa wameanzisha jukwaa la kijamii la kidigitali la mawasiliano ambapo wananchi wanaweza kupokea taarifa za tahadhari za mapema kuhusu maafa au kupewa taarifa bure kuhusu maafa katika eneo lolote.

“Kwa mfano wenye simu zenu hapa sasa hivi, unaweza kuchukua simu yako ukaandika *190# utaona mwenyewe itakupeleka karibu Ofisi ya Waziri mkuu inakuuliza umepatwa na changamoto gani pengine kama ni ajali au mafuriko au mengineyo unaeleza kila kitu hapo ili kwa pamoja tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kwa haraka,”amesema Mhe. Nderiananga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwandamizi wa World Vision Tanzania Dkt. Joseph Mayala amesema kuwa wao shirika la kimataifa wanahakikisha viongozi wa dini wanashirikishwa katika mikakati yote inayohusiana na suala la kukabiliana na maafa nchini kwani wana ushawishi mkubwa katika jamii.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Manejimenti ya Maafa (RAPID) Taniel Mkongo amesema kuwa kauli mbiu ya leo katika maadhimisho hayo inatokana na mkakati wa sendai wa kupunguza madhara ya maafa wa 2015-2030 ambao unataka kushughulikia sababu za msingi za madhara ya maafa.

“Tunajua kuwa mara nyingi watu maskini na walio hatarini zaidi wanapata athari kubwa za maafa na wanakabiliwa na athari kubwa zaidi, kupambana na kutokuwiana ni sehemu muhimu ya kujenga mustakabali wa kustahimili kupunguza athari za maafa,”amesema.

Siku ya kimataifa ya kupunguza maafa ilianza mwaka 1989 baada ya wito kutoka kwa Baraza la Umoja wa Mataifa kutaka kuwepo kwa siku hii maazimio Na. 64/200  Desemba 21,2009 ilinayohitaji watu na jamii zote duniani kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kudhibiti madhara ya maafa.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga akizungumza Katika kongamano la maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupunguza madhara ya Maafa Leo Jijini Dodoma

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...