Shirika la kuhudumia viwanda vidogo Tanzania (SIDO) limewatunuku vyeti wafanyabiashara 110 wanaomiliki viwanda vidogo mkoa wa Dar es salaam ili kuendelea kuwatambua na kuwahudumia kirahisi chini ya mamlaka hiyo.

Akizungumza baada ya zoezi hilo Mkuerugenzi wa fedha na Utawala wa SIDO Bw. Muhamed Kitara amesema vyeti hivyo vinaisaidia serikali na mamlaka za viwanda kuwatambua na kuwaendeleza na kupitia SIDO serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi Kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wote ili waweze kufanya Biashara zao Kwa urahisi

Naye Kaimu meneja wa SIDO mkoa wa Dar es salaam Melkiado January amesema SIDO imekuwa na utaratibu wa kuwatambua na kuwatunuku vyeti wanaviwanda ili kuwatambua kulingana na kada zao ili kurahisha utoaji huduma na kuwapa uhuru wa kufanya Biashara zao bila usumbufu wowote.

Lengo kubwa la kuwatambua wanaviwanda Hawa ni kuwapa uhuru na kupitia vyeti hivi vinawapa uwezo wa kufanya kazi na tasisi zote za serikali zikiwemo za kifedha ili waweze kuhudumia kirahisi Zaidi. Amesema Bw. January

Bw. January ameongeza kuwa SIDO imekusudia kuwafikia wanaviwanda wote wa mkoa wa Dar es salaam ili kurahisisha ufatiliaji na utoaji huduma pale wanapohitajika ili kulinda maendeleo ya viwanda hivyo.

Mmoja wa wanaviwanda walipokea vyeti hivyo Bi. Diana Mwalimu kutoka Mtwara K industries ameshukuru SIDO Kwa kuendelea kuwatambua na kupitia vyeti hivyo wanaweza kujitangaza na kujenga Imani kubwa Kwa wateja na wadau wengine wa secta hiyo ya viwanda



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...